Miradi ya kukijanisha
Singida, Tanzania
Singida, Tanzania

Kazi
Kuongoa ardhi iliyoharibika kwa kilimo cha kuzalisha uoto upya, kunatengeza tija katika maisha ya vijijini
Katika mikoa ya Amhara (Gubalafto) na Oromia (ya kati Awash) nchini Ethiopia, mshirika wetu MetaMeta analenga kuimarisha uchumi wa ndani, a vijijini.
Kwa kurejesha mandhari ya ardhi kwa njia ya kuzuia maji na kudhibiti mmomonyoko wa ardhi, kuanzisha mbinu za kilimo cha kurejesha uoto, na kutoa uelewa na mvuto kwa fursa za maisha ya vijijini ambazo hazijatumika (mfano ufugaji wa kuku, uzalishaji wa mbolea ya mimea/viwatilifu na masoko) wanawaonyesha wanajamii jinsi wanavyoweza kuongeza kipato chao.
Mikoa hii miwili inatofautiana katika masuala ya jiolojia, udongo, hali ya hewa, na namna ya kufanya kilimo. Kwa sababu hii, mradi unashughulikia masuala mbalimbali na unaonyesha aina mbalimbali za ufumbuzi. Shughuli kufikia sasa ni pamoja na: mafunzo kwa ajili ya uzalishaji wa mbolea ya mimea, kuanzisha vitalu vya miti inayoongozwa na vijana, kusaidia kampeni za serikali za kuongoa mazingira, kurejesha na kukijanisha ardhi iliyoharibia kupitia kilimo cha kurejesha uoto tena.
Justdigit inasaidia mradi huu kupitia wataalamu wa vyombo vya habari, mawasiliano na kubadili tabia.
watafaidika
zitarejeshwa
Mradi huo utawafikia watu 11,200 huko Gubalafto na Awash ya Kati, ambapo zaidi ya watu 7,000 ni wanawake. Watafaidika kutokana na kuongezeka tija katika maisha ya vijijini, yaliyotengenezwa na mradi huo.
Justdiggit hutumia vyombo vya habari na mawasiliano ili kuongeza athari ya (kiwango kikubwa) katika urejeshaji wa mandhari.
Kwa miaka mingi tulipata ujuzi na uzoefu mwingi wa jinsi ya kuendeleza na kutekeleza mbinu tofauti za mawasiliano na kuunda mtandao mkubwa wa washirika wa vyombo vya habari duniani kote. Kwa uwezo huu wa vyombo vya habari na mawasiliano, sasa tunasaidia MetaMeta na miradi yao katika Gubalafto na Awash ya Kati. Kwa mfano, tulitengeneza vipeperushi kwa wakulima wadogo kuhusu jinsi ya kutengeneza mbolea ya mimea kwenye mashamba yao, ili kuimarisha rutuba ya udongo, kuongeza mavuno ya mazao yao.
Mandhari ndani ya mkoa wa Amhara
Miradi ndani ya Gubalafto na Awash ya kati ni sehemu ya Kilimo cha kijani kijacho katika programu na juhudi za RAIN, MetaMeta na Justdigit. Kilimo cha kijani ya baadaye ni mradi wa miaka minne unaolenga kuonyesha jinsi gani katika mandhari tatu tofauti kabisa, katika nchi tatu tofauti (Uganda, Ethiopia na Kenya), kilimo cha urejeshaji wa uoto kinaweza kuwanufaisha wakulima na mazingira. Kwa kuchanganya uwekezaji katika kuongoa wa uoto wa asili na usimamizi wa mandhari, kujumuisha kilimo cha kurejesha uoto, na kuimarisha minyororo ya thamani ya ndani, mradi unalenga kufanya uchumi wa vijijini kuwa na nguvu zaidi.
Kinachofanya programu kuwa maalum ni ukweli kwamba kila shirika sio tu linaendesha programu yao ya ndani, lakini pia inasaidia programu zingine ndani ya utaalam wao wenyewe. Lengo kuu la programu ni kujenga mustakabali wa mandhari ya kijani kwa wengi, haswa kwa wanawake na vijana, katika sehemu tofauti za Afrika Mashariki. Mpango huu unaungwa mkono na IKEA Foundation.
Tazama filamu ya utangulizi Kilimo cha Kijani ya Baadaye hapa.