Donate
Airmiles

Dodoma Tanzania

Kwa kutumia mbinu ya Kisiki Hai na kuanzisha upya mbinu ya kuvuna maji ya mvua, tunalenga kurejesha ardhi, kurudisha uoto asili na kuboresha uzalishaji wa ardhi mkoani Dodoma, Tanzania. Kwa mradi wetu tutafikia vijiji 300 katika kada ya Dodoma, na hivyo kusaidia watu 900,000

Design Phase
100% done
Implementation Phase
15% done
180,000
hekta za kukijanisha
Maji
kuboresha upatikanaji vijijini
900,000
Watu (2020)
Kiwango cha joto
kupungua
01

Kukijanisha na wakulima wa Tanzania

Dodoma ni moyo wa Tanzania, na nyumbani kwa mji mkuu. Ina ukubwa wa kilomita za miraba 41,311 inakaibia ukubwa wa Uholanzi. Idadi ya watu ni 2,083,588 (2012), ambayo 90% inategemea ardhi kwa ajili ya maisha.  Ardhi inatumika kwa ajili ya kilimo na ufugaji. 

Ingawa jamii katika eneo la Dodoma (eneo kame)  zimeonyesha ujasili kuishi katika  mazingira na hali ya hewa ngumu, tatizo la ukataji  miti, uharibifu wa ardhi na mabadiliko ya hali ya hewa imeendelea kwa kiwango cha kutisha, hivyo kuharibu uwezo wa mazingira wa kuendeleza viumbe hai na kutoa rasilimali za asili za maji na udongo wenye rutuba.

Ili kuboresha maisha ya watu na ustahimili wa hali ya hewa katika mkoa wa Dodoma, tulishirikiana na LEAD foundation kama sehemu ya lengo la mwisho la kukijanisha Tanzania. Mwaka 2017, eneo la programu hii lilichaguliwa  na kufanya muundo wa mradi. Itatekelezwa kwanza katika kanda ya Kongwa, sehemu ya mashariki ya mkoa wa Dodoma, Hii tayari ilianza Desemba 2017.  Mnamo mei 2018, programu itaanzishwa katika mkoa mzima wa Dodoma.

Pamoja na washirika wetu LEAD Foundation na MetaMeta na jamii tumechagua hatua zitakazozingatia kipindi kijacho. Mpango huu utahusisha njia mbili; Kisiki Hai na njia ya kuvuna maji ya mvua. Mpango huu utahusisha njia mbili.

04

We'd love to hear from you

Questions, ideas, suggestions or just to say ‘Hello’. Drop us a note! We will get back to you as soon as possible.

Visiting address
Justdiggit
Prins Hendrikkade 25
1012 TM Amsterdam
The Netherlands

Tel. +31 (0)20 737 23 66
Mail. info@justdiggit.org

IBAN. NL59 RABO 0160 3724 88
SWIFT. RABONL2U