JUKWAA LA UKIJANISHAJI KIDIGITALI
Kuwezesha wakulima milioni 350 kukijanisha ardhi zao
HAMASISHA UKIJANISHAJI
Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita tumefanikiwa kurejesha uoto kwenye maelfu ya hekta za ardhi, tumechimba mashimo ya kuhifadhia maji takribani nusu milioni, na tumerejesha miti milioni 18 kwa kutumia mbinu za ukijanishaji za teknolojia ya chini. Kimsingi, hii ni kazi nzuri sana, lakini bado haitoshi. Sasa ni wakati wa kuhamasisha zaidi kazi hii. Hebu tukujuze: mbinu za ukijanishaji za kidigitali.
Kuongezeka kwa simujanja zenye uwezo wa intaneti pamoja na huduma ya mtandao huo katika ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara, kunatoa fursa ya kutumia jimujanja hizo katika kuharakisha urejeshaji wa uoto. Hivyo, kwa kuandaa Ukurasa wa Kidigitali kwa ajili ya Ukijanishaji, tunaweza kuendeleza na kuongeza kasi ya ukijanishaji, hali inayotufikisha karibu na kutimiza lengo letu la kuwafikia wakulima wadogowadogo milioni 350.
KIJANI
Kitovu cha jukwaa hili la kidigitali ni Kijani, hii ni app inayowapa wakulima walioko ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika, maarifa na ujuzi unaohitajika kwa ajili ya kukijanisha ardhi zao kwa ufanisi. Aidha, wanaweza kufuatilia masomo ya kidigitali yenye mbinu zilizothibitishwa ili kukijanisha ardhi zao na kuboresha maisha yao.
Kipekee kabisa, tunaishukuru teknolojia ya GPS, kwani tunaweza kutoa ushauri mahususi kabisa kwa kila mtumiaji wa app, jambo linalotufanya tuelimishe wakulima wengi zaidi bila hata sisi kwenda katika maeneo yao. Kwa kutumia jukwaa hili, tunaweza kutumia vizuri fursa ya uvumbuzi mkubwa wa kiteknolojia katika kuendeleza mipango ya ukijanishaji inayotumia teknolojia ndogo.
“Mara nyingi mashirika hutoa elimu na kisha hutoweka, lakini app hii ni chaguo sahihi sana. Ninaweza kupakua app hii na inaendelea kubakia kwenye simu yangu. Sasahivi nina nafasi nzuri ya kujifunza leo na kesho,”
“WAKATI MABILIONEA WA TEKNOLOJIA WAKIENDA SAYARI YA MIRIHI, SISI KIPAUMBELE CHETU NI ‘KUOKOA DUNIA’. KUPITIA TEKNOLOJIA, TUNAWAWEZESHA WAKULIMA MILIONI 350 KUKIJANISHA AFRIKA.”