Miradi ya kukijanisha
Gubalafto na Awash ya kati, Ethiopia
Gubalafto na Awash ya kati, Ethiopia

Kazi
Kuongoa mashamba ya kahawa kwa kutumia kilimo cha krejesha uoto tena
Kwa kutekeleza kilimo cha kurejesha uoto, mshirika wetu RAIN analenga kurejesha uoto katika mashamba ya kahawa kwenye miteremko ya kaskazini ya Mlima Elgon, Uganda.
Miteremko ya kaskazini ya Mlima Elgon ina sifa ya mandhari ya milima yenye udongo wenye rutuba wa volkano. Wakulima katika eneo hilo hutegemea sana udongo huu wenye rutuba kwa maisha yao.
Hapo awali wakulima wengi katika eneo hilo walitumia ardhi yao kuzalisha kahawa ya Arabica. Hata hivyo, kutokana na bei ya chini ya kahawa na ukosefu wa upatikanaji wa masoko ya kahawa, wakulima wengi walihamia katika uzalishaji wa mazao ya kila mwaka. Mazao haya hayafai kwa mandhari ya Mlima Elgon yenye vilima kwani mara nyingi husababisha uharibifu wa mazingira kama vile mmomonyoko wa udongo, uharibifu wa kingo za mito na kuchafua udongo na rasilimali za maji.
Kupitia kutekeleza njia za urejeshaji wa mandhari (kama vile uimarishaji wa ukingo wa mto kwa kupanda mianzi) na mbinu za kulima kwa kurejesha uoto (kama vile matandazo, kuchimba mtaro tuta na kutumia mbolea ya asili kutoka kwa mabaki), mandhari inaweza kurejeshwa. Wakati huo huo, kuboresha uzalishaji wa kahawa na kuendeleza uhusiano wa soko la kahawa kunaweza kugeuza kahawa kuwa fursa ya faida kwa wakulima tena. Justdiggit inaunga mkono mradi wa Mlima Elgon kwa utaalam wake kwenye vyombo vya habari na mawasiliano.
za ardhi iliyorejeshwa
zaidi ya mapato kwa wakulima
wa kahawa ya Arabica
Kwa jumla, hekta 33,000 za ardhi zitazalishwa upya, na kutengeneza mashamba yenye ubora kwa ajili ya uzalishaji wa kahawa.
Mandhari iliyorejeshwa huongeza tija ya mashamba ya kahawa na hivyo uzalishaji wa kahawa ya Arabika. Kadiri wakulima wanavyozalisha kahawa kwa wingi na kupata soko la kahawa, mapato yao yataongezeka kwa asilimia 20.
Ardhi iliyorejeshwa hairuhusu tu kahawa zaidi ya Arabica kuzalishwa, pia inaboresha ubora wa kahawa.
Justdiggit hutumia vyombo vya habari na mawasiliano ili kuongeza athari ya (kiwango kikubwa) katika urejeshaji wa mandhari.
Wakulima wa kahawa wanachimba mitaro tuta katikati ya mazao kuvuna maji ya mvua
Mradi huo kwenye Mlima Elgon ni sehemu ya mpango wa Kilimo cha Kijani ya baadaye, mpango kutoka RAIN, MetaMeta na Justdiggit. Kilimo cha kijani ya baadaye ni mradi wa miaka minne unaolenga kuonyesha jinsi gani katika mandhari tatu tofauti kabisa, katika nchi tatu tofauti (Uganda, Ethiopia na Kenya), kilimo cha urejeshaji wa uoto kinaweza kuwanufaisha wakulima na mazingira. Kwa kuchanganya uwekezaji katika kuongoa wa uoto wa asili na usimamizi wa mandhari, kujumuisha kilimo cha kurejesha uoto, na kuimarisha minyororo ya thamani ya ndani, mradi unalenga kufanya uchumi wa vijijini kuwa na nguvu zaidi.
Kinachofanya programu kuwa maalum ni ukweli kwamba kila shirika sio tu linaendesha programu yao ya ndani, lakini pia inasaidia programu zingine ndani ya utaalam wao wenyewe. Lengo kuu la programu ni kujenga mustakabali wa mandhari ya kijani kwa wengi, haswa kwa wanawake na vijana, katika sehemu tofauti za Afrika Mashariki. Mpango huu unaungwa mkono na IKEA Foundation.
Tazama filamu ya utangulizi Kilimo cha Kijani ya Baadaye hapa.