HATUA 1: Angalia
Baini uelekeo wa mtiririko wa maji katika shamba lako kwa kuangalia au kwa kutumia vipimo.
- Fikiria sehemu ambayo ungependa kuweka Fanya Juu au Fanya Chini ili kuzuia mtiririko wa maji.
- Kwa kawaida, huwa kuna umbali wa mita 10 mpaka 20 kati ya kingamaji moja la Fanya Juu au Fanya Chini na kinga maji lingine kulingana na kasi ya mteremko. Idadi na mpangilio wa makinga maji hupatikana wakati wa upimaji.
- Hakikisha angalau una kingamaji moja upande wa juu la shamba lako na lingine upande wa chini ya shamba lako, lakini idadi hii yaweza ongeza kulingana na kasi ya mteremko.