Cooling Down
the Planet
Together
TUNACHOKIFANYA KINAFANIKIWA.
Justdiggit hutumia njia za kiasili kukijanisha ardhi iliyoharibiwa.
Kwa kushirikiana na wakulima, wakazi wa maeneo husika na wadau wa ndani, tunaimarisha mifumo ya ekolojia kwa kiasi kikubwa kwa kurejesha miti, kuchimba makinga maji na kuhakikisha uwepo wa hifadhi ya mbegu za nyasi. Hivi ndivyo tunavyosaidia kujenga jamii zinazoweza kupambana na tabianchi, kuongeza bayoanuwai – na hatimaye kupunguza joto la sayari yetu. Je, ungependa uungane nasi katika huu mpango wetu? Karibu!
Hadithi ya Justdiggit
MBINU ZA KUBADILISHA ARDHI KAME KUWA KIJANI
Kukijanisha si suluhisho pekee.
Kuna mbinu mbalimbali ambazo ni nzuri kutumika katika usimamizi wa ardhi. Ndiyo maana, katika miradi yetu tunatumia mbinu tofautitofauti za uboreshaji wa mazingira. Hizi ni mbinu tatu ambazo hutumika mara nyingi: