Miradi ya kukijanisha
Kuku, Kenya
Kazi
Kurejesha nyanda za malisho zilizoharibiwa na kuhamasisha matumizi endelevu ya ardhi
Pamoja na Jumuiya ya Wamiliki wa Ardhi ya Kusini mwa bonde la ufa tunarejesha nyanda za malisho zilizoharibiwa katika Mkoa wa Kusini mwa bonde la Ufa na kuhimiza jamii kutekeleza tamaduni ya matumizi endelevu ya ardhi. Kwa kurudisha uoto na kulinda nyanda za malisho tunaweza kuboresha maisha ya jamii ya Wamasai na kusaidia wanyamapori wanaoishi katika eneo hilo.
Eneo la Kusini mwa bonde Ufa ni sehemu ya Bonde la Ufa Kusini, lililo karibu na mpaka wa Tanzania. Eneo hilo liko karibu na hifadhi kubwa mbili za wanyamapori – Serengeti-Mara na Kilimanjaro Mkuu-Amboseli-Tsavo – na inasaidia baadhi ya wanyama wenye utajiri zaidi duniani. Ni nyumbani kwa wafugaji wa Kimasai: jamii ya kuhamahama ambayo chanzo chake kikuu cha mapato na maisha ni ufugaji. Kwa sababu ya ukame unaoendelea, malisho ya mifugo kupita kiasi, na ongezeko la aina mbalimbali za hatari za mimea vamizi, maeneo ya malisho na vyanzo vya maji kwa mifugo yao vinapungua. Wakati huo huo, wanyamapori katika eneo hilo pia wanajitahidi kujikimu.
Wakati wa kuchukua hatua! Pamoja na mshirika wa SORALO tunatekeleza mbinu mbalimbali za kurejesha mandhari ili kurudisha uoto endelevu katika eneo hilo na kuondoa viumbe vamizi. Kwa kukuza mazoea ya matumizi endelevu ya ardhi miongoni mwa jamii, tunalenga kuboresha ubora wa nyanda zao za malisho. Hii itasababisha usalama zaidi wa chakula na maji, lishe zaidi kwa mifugo yao, na mapato zaidi kwa jamii zinazoishi katika eneo hilo. Kwa kuongezea, itasababisha makazi bora kwa wanyama wanaoishi katika mkoa huo. Kwa kiwango kikubwa, kufanya ardhi iliyoharibiwa kuwa ya kijani kibichi kuna athari ya kupoeza kwa hali ya hewa (ya ndani).
wa mahitaji na ustahimilivu
zenye afya
kwa bioanuwai
hali ya hewa
Kurejesha nyanda za malisho zilizoharibiwa kunasababisha upatikanaji wa chakula na maji zaidi, malisho mengi ya mifugo na mapato zaidi kwa jamii ya Wamasai wanaoishi katika eneo hilo.
Kwa kurudisha uoto, kuondoa aina za mimea vamizi zisizohitajika na kurejesha rasilimali za maji, tunaboresha ubora na afya ya nyanda za malisho katika Mkoa wa Kusini mwa bonde la Ufa.
Kwa kurejesha nyanda za malisho zilizoharibiwa, pia tunaboresha hali ya maisha ya aina nyingi tofauti za wanyama na mimea.
Mimea tunayorudisha kwenye nyanda za malisho hupooza mazingira moja kwa moja kupitia kuvukiza na kutoa kivuli. Pia katika kiwango cha meso huathiri hali ya hewa, kwani mimea huvuna kiasi kikubwa cha CO2 kutoka angani.
Kwa kutekeleza mbinu mbalimbali za kurejesha mandhari tunarudisha uoto endelevu kwenye nyanda za malisho. Mbinu zilizopendekezwa ni:
Mbinu zilizotekelezwa zitasaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo wenye rutuba na kurejesha ulinganifu wa maji katika udongo.
Pia tutavuna maji kama suluhisho la usimamizi wa malisho. Kwa kutoa maji mengi zaidi nje ya maeneo ya malisho yaliyohifadhiwa, mifugo inaweza kuwekwa nje ya maeneo hatarishi kwa muda mrefu, na hivyo kuacha muda zaidi kwa mimea kurejea.
Hifadhi ya mbegu za nyasi ni sehemu ndogo ya ardhi ya jumuiya ambayo hutumiwa kwa ajili ya uzalishaji wa nyasi na mbegu za nyasi.
Hifadhi ya mbegu za nyasi zinasimamiwa na kudumishwa na vikundi vya wanawake wa Kimasai. Mara baada ya nyasi kuota kikamilifu, nyasi huzalisha mbegu za nyasi ambazo huuzwa na wanawake katika masoko ya ndani au kwa miradi mingine ya kukijanisha. Hii inamaanisha mapato zaidi kwa wanawake na kijani zaidi katika maeneo mengine, hali ya ushindi!
Ili kuhakikisha uendelevu wa miradi, tutatengeneza mpango wa usimamizi wa malisho pamoja na mshirika wetu wa ndani na jamii.
Lengo ni kuzuia malisho ya mifugo kupita kiasi katika maeneo muhimu na hatarishi ya malisho.
Mradi huo ulioko kusini mwa bonde la ufa ni sehemu ya kilmo cha kijani cha badae cha kijani, juhudi kutoka RAIN, MetaMeta na Justdiggit.Kilimo cha kijani ya baadaye ni mradi wa miaka minne unaolenga kuonyesha jinsi gani katika mandhari tatu tofauti kabisa, katika nchi tatu tofauti (Uganda, Ethiopia na Kenya), kilimo cha urejeshaji wa uoto kinaweza kuwanufaisha wakulima na mazingira. Kwa kuchanganya uwekezaji katika kuongoa wa uoto wa asili na usimamizi wa mandhari, kujumuisha kilimo cha kurejesha uoto, na kuimarisha minyororo ya thamani ya ndani, mradi unalenga kufanya uchumi wa vijijini kuwa na nguvu zaidi.
Kinachofanya programu kuwa maalum ni ukweli kwamba kila shirika sio tu linaendesha programu yao ya ndani, lakini pia inasaidia programu zingine ndani ya utaalam wao wenyewe. Lengo kuu la programu ni kujenga mustakabali wa mandhari ya kijani kwa wengi, haswa kwa wanawake na vijana, katika sehemu tofauti za Afrika Mashariki. Mpango huu unaungwa mkono na IKEA Foundation.
Tazama filamu ya utangulizi Kilimo cha Kijani ya Baadaye hapa.