NINI MAANA YA MABADILIKO YA
HALI YA HEWA?

Tunasikia zaidi na zaidi: hali ya hewa inabadilika. Lakini hii inamaanisha nini?

Hali ya hewa inaonekana kama hali ya hewa ya kawaida katika eneo fulani. Kwa mfano, hali ya joto katika Amazon mara nyingi  ni kubwa na inanyesha karibu kila siku, wakati kwenye Antaktika daima kuna baridi na karibu hakuna mvua. Wakati joto la kawaida na kiwango cha mvua katika eneo maalum hubadilika, kuna mabadiliko katika hali ya hewa ya kawaida. Haya ni mabadiliko ya hali ya hewa. Sio tu katika maeneo maalum mabadiliko ya hali ya hewa yanaonekana, ulimwenguni kote athari za mabadiliko ya hali ya hewa zinaonekana.

SABABU NA MATOKEO

Nini kinasabisha mabadiliko ya hali hewa?
Nini matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani?

NINI MAANA YA MABADILIKO YA
HALI HEWA?

Mabadiliko katika hali ya hewa sio jambo geni.

Hapo zamani, sababu za asili, kama milipuko ya volkano na El Niño, zilisababisha kushuka kwa joto na mvua. Kilicho kipya, ni ushawishi wa wanadamu juu ya mabadiliko ya hali ya hewa. Tunaendesha magari yetu, tunapasha moto nyumba zetu wakati nje ni baridi, na tunatumia nishati kupika. Shughuli hizi za kila siku husababisha  gesi chafu, kama vile methane na kaboni. Gesi hizi huzuia joto linalotolewa na dunia kupita, na kusababisha ongezeko la joto duniani.

Climate change CO2 emissions Chimney Justdiggit

Nini matokeo ya mabadiliko ya
hali ya hewa duniani?

Ongezeko la joto duniani lina matokeo mbalimbali.

Mawimbi ya joto hutokea mara nyingi zaidi, mvua huwa kali zaidi na kina cha bahari kinaongezeka. Hasa ndani ya maeneo hatarishi, kama Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa huonekana kila siku. Joto kali na ukosefu wa mvua husababisha ukame, na kutopata mazao kama matokeo. Mvua inapowadia, mvua huwa kubwa sana, bila kuacha wakati wa maji kupenya kwenye udongo, na kusababisha mafuriko kwenye maeneo ya miteremko, kuondoa safu ya juu yenye rutuba ya udongo. Mchakato unaoitwa mmomomyoko. Inasababisha uharibifu wa ardhi, na kufanya iwe ngumu kukuza mazao, na kusababisha kupungua kwa mimea na kudumisha ardhi kuwa kavu. Hii inaweza kusababisha uhaba wa chakula kwa jamii za wenyeji. Kwa kuwa hawahakikishiwi kupata chakula, watu wanahamia maeneo mengine, wakitumaini kupata udongo wenye rutuba ambapo wanaweza kukuza mazao yao. Watu hawa pia huitwa wakimbizi wa  athari za kimazingira. Wanalazimika kukimbia kutokana na matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Climate change - drought in Africa - Justdiggit
Water bunds landscape restoration Justdiggit Cooling effect vegetation

JINSI TUNAVOWEZA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA HALI YA HEWA?

Tunaweza kufanya hivi kwa  msaada wa Kukijanisha.  Uchunguzi wa hivi karibuni unaonyesha kuwa njia za asili zinaweza kuchangia hadi 37% ya ufyonzaji wa hewa chafu ya kaboni inayohitajika kuweka joto la joto chini ya digrii 2 za nyuzi joto. Mimea husababisha kufyonzwa wa kaboni, na kupunguza kiwango cha kaboni angani na baadaye kupunguza athari ya hewa chafu, mwishowe kusababisha upunguzaji wa joto duniani. Mimea pia husababisha baridi kwenye udongo, na kupunguza uvukizi wa maji kutoka kwenye udongo na kusababisha kuongezeka kwa upatikanaji wa maji kwa mimea, wanyama na wanadamu. Kwa kuongezea, kijani kibichi huchochea mzunguko wa maji, na kusababisha kuongezeka kwa mvua na utunzaji wa maji kwenye udongo. Kuongezeka kwa kiwango cha unyevu wa udongo hufanya ardhi kuwa tayari kwa kilimo tena, ikichangia upatakinaji chakula na kipato  kwa jamii za wenyeji.

Ni nani Justdiggit?

Na Jinsi gani Justdiggit wanasaidia kupambana na kutoa gesi ya kaboni na kupoooza sayari?

Justdiggit ni shirika la Uholanzi likiwa na lengo la kurejesha mifumo ya mazingira iliyoharibika kwa kukuza, kuanzisha na kufadhili mipango mikubwa ya urejesho wa mazingira ndani ya Afrika. Miradi yetu ya kukijanisha husaidia kurejesha ulinganifu wa maji kwenye udongo na kurudisha mimea, ambayo ina athari nzuri kwa hali ya hewa ya eneo , inaongeza usalama wa maji na chakula na inakuza bioanuwai ndani ya maeneo ya mradi. Ndani ya miradi yetu tunafanya kazi pamoja na washirika wa ndani na jamii. Jamii zilizohusika moja kwa moja zinanufaika na programu zetu tunapounda mazingira bora ya kuishi na kuongeza maendeleo ya uchumi. Njia yetu ya kipekee ni mkakati wa vyombo vya habari na mawasiliano, unaojumuisha mawasiliano na vyombo vyote vya habari vinavyopatikana kwa kiwango cha mitaa, mkoa, kitaifa na kimataifa. Pamoja na kampeni hizi za vyombo vya habari zilizodhaminiwa, tunakusudia kukuza athari ya programu za urejesho wa mazingira, na hivyo kuunda harakati za kurudisha mazingira, na kukuza kukijanisha barani Afrika.

poster