KUPANUA WIGO WA KUKIJANISHA
MTI KWA MTI

Baada ya kufanikiwa kurudisha mamilioni ya miti katika mkoa wa Dodoma, tunapanua wigo wetu na kuongeza ukuaji wa kukijanisha kwa mkoa wa jirani wa Singida kuanzia Mei 2021 na kuendelea.

Mkoa wa Singida upo Magharibi mwa Dodoma na ndiko nyumbani kwa wakulima wadogo wadogo, ambao wanategemea sana ardhi ya kijani kibichi na yenye rutuba kukuza mazao yao. Wakulima wazee katika mkoa wanasimulia hadithi kuhusu jinsi mazingira yao ya kuishi yalivyokuwa ya kijani kibichi. Kwa miaka mingi, hata hivyo, mandhari haya ya kijani yamepotea kwa sababu ya ukataji miti, uharibifu wa ardhi, na mabadiliko ya hali ya hewa. Kilichobaki ni eneo tasa na kavu ambapo wakulima wanajitahidi kukuza mazao yao.

Muda wa vitendo: Kwa msaada wa Njia ya Kisiki Hai na Uvunaji wa maji ya mvua wakulima wanaweza kuifanya ardhi yao kuwa ya kijani na yenye rutuba tena. Pamoja wanaweza kurejesha na kutunza mamilioni ya miti na kuvuna mabilioni ya lita za maji , kurejesha ardhi kavu na mandhari iliyoharibika ya mkoa wa Singida. Programu hii ilianzishwa na kutekelezwa na washirika wetu LEAD Foundation.

MATARIJIO YA ATHARI
MWAKA 2026

8 million +

Miti milioni 8 kurejeshwa

± 100,000

Zaidi ya watu laki moja watawezeshwa

ZAIDI YA MITI MILIONI NANE KUREJESHWA

Tunarejesha visiki vya miti iliyosahaulika kwa kutumia njia ya Kisiki Hai. Njia hii ni ya uhakika zaidi kuliko kupanda miti. Kwa kujinanisha miti hio tunaweza kuongoa eneo lililoharibika na maeneo hayo kuwa ya kijani na yaliyopoa tena.

2_techniques_landscape restoration_what we do_Justdiggit_Kisiki Hai_mnya_Tanzania

ZAIDI YA WATU LAKI MOJA WATAWEZESHWA

Kuwawezesha watu, mmoja mmoja, kuirudisha ardhi yao ni njia ya gharama nafuu na ya ukubwa  na ni kichocheo cha mabadiliko ya kijamii na kiuchumi. Ili hili lifanyike tunahitaji kuingia ndani ya mioyo na akili za watu. Tunawahamasisha wakulima kwa kuonyesha faida za kurejesha ardhi na kuwapa zana za jinsi ya kuanza.

Kisiki Hai 2 - Tanzanian version.mp4.00_17_31_02.Still001

Njia yetu

Kisiki Hai
Fanya Juu na Fanya Chini
Kuwajengea uwezo
Kuanzisha Harakati
Kukijanisha kwa umbali

Kisiki Hai

Kisiki Hai ni njia ya kukuza maotea ya miti na kuwezesha maotea ya asili kuchipua na kukua. 

Pamoja na LEAD Foundation tunawafundisha wakulima kutumia njia  hiyo katika mashamba yao ambapo itasadia mamilioni ya miti kurejea , kukijanisha sio tu mashamba yao bali pia mkoa mzima wa Singida. 

Unataka kujifunza zaidi juu ya njia Kisiki Hai na faida zake?

What we do Treecovery

Fanya Juu na Fanya Chini

Fanya Juu na Fanya Chini ni mbinu ya kuvuna maji ya mvua. Wakulima huchimba mitaro ndani ya mashamba yao ili kuzuia mmomonyoko na kuvuna maji ya mvua yenye thamani ndani ya ardhi yao.

Fanya Chini maana yake ni ‘tupa chini’ kwa Kiswahili. Inazuia  maji ya mvua kutoka nje ya shamba kuingia shambani, kuzuia mmomonyoko wa udongo wenye rutuba. Fanya Juu inamaanisha ‘tupa juu’, na inazuia maji ya mvua kutoka ndani ya shamba kukimbia, na kuongeza upatikanaji wa maji kwa mazao kwenye ardhi. Mwishowe, inasaidia wakulima kukijanisha mashamba yao hata zaidi!

Unahitaji kujua zaidi kuhusu faida za mbinu hizi?

Digging Fanya Juu Fanya Chini

Kuwajengea uwezo

Kwa kufundisha wawezeshaji 800 , tunaweza kufikia vijiji 200 ndani ya  mkoa waSingida.

Wakulima hao wa mfano hufundisha wanajumuiya wenzao juu ya jinsi ya kurejesha miti kwenye ardhi yao. Kwa njia hii maelfu ya watu wamehamasishwa kukijanisha ardhi zao wenyewe, na kurudisha mamilioni ya miti katika mkoa wa Arusha na kusababisha kuongezeka kwa uwezo wa kupambana na ukame, uzalishaji wa chakula, na mapato ya kaya. Wakulima hao wa mfano wa pia wamefundishwa kuhusu  uvunaji wa maji ya mvua, ikiwasaidia kukijanisha ardhi hata zaidi.

Video Tour Dodoma_Marc Hears

Kuanzisha Harakati

Kwa sisi sio muhimu tu kufundisha watu jinsi ya kukijanisha ardhi zao, lakini pia kutafuta njia zingine za kuzifikia na kuwapa msukumo. Kwa kujenga harakati halisi ya kukijanisha tunakusudia kufikia na kuhamasisha mamilioni ya wakulima ndani ya mkoa wa Singida.

Sehemu ya harakati hii ya kukijanisha ni maonyesho yetu ya sinema: msafara wa video unaenda kutoka kijiji hadi Kijiji na kufikia vijiji 200. Maonyesho ya barabarani ni hafla ya siku nzima, iliyojaa michezo, muziki, dansi, na maonyesho yote kuhusu Kisiki Hai. Wakati wa jioni, sinema kubwa inawekwa, ambayo inaonyesha sinema ya kuvutia ya Kisiki Hai ambayo imetengenezwa kabisa  ndani ya katikati ya Tanzania.

Movie roadshow Tanzania

Kukijanisha kwa umbali

Ili kueneza harakati ya kukijanisha hata zaidi, tumeanzisha njia anuwai za kufikia na kuamsha jamii, bila kuwatembelea kimwili. Kwa njia hii tunaweza kuhamasisha wafugaji na wakulima ndani na nje ya mkoa wa Arusha!

Pamoja na washirika wetu LEAD na Climate Edge, tutatoa huduma ya kutuma ujumbe mfupi. Wafugaji wanaweza kujiunga na huduma hii, ambayo itawatumia ujumbe mfupi kila wiki na vidokezo na ujuzi wa jinsi ya kutumia njia ya Kisiki Hai na Fanya Juu, na Fanya Chini.

sms service

DHAMIRA YETU

Dhamira yetu ni kuibadilisha Afrika katika miaka 10 ijayo, pamoja na mamilioni ya wakulima, na pamoja na wewe.

If we want to cool down the planet in one decade, everyone needs to be in on the change. We use the power of media, communication, data, and the latest technology to spread our message and scale-up. We want to inspire, unite and empower an entire generation, growing a landscape restoration movement.

Ikiwa tunataka kupooza sayari kwa muongo mmoja, kila mtu anahitaji kuwa kwenye mabadiliko. Kupitia nguvu ya vyombo vya habari, mawasiliano, taarifa, na teknolojia ya kisasa tunaweza kueneza ujumbe wetu na kuongeza kiwango. Tunataka kuhamasisha, kuunganisha na kuwezesha kizazi kizima, kukuza harakati za kurudisha mazingira.

KAZI NYINGINE

Kazi zetu zote