JUSTDIGGIT NDANI
YA UHOLANZI

Justdigit walianza kampeni ndani ya uholanzi mwaka 2013

Kampeni ya kwanza ilikuwa kuzindua chapa ya Justdiggit na kuonyesha moja wapo ya suluhisho la mabadiliko ya hali ya hewa: kuchimba. Mshirika wetu Desmond Tutu aliigiza katika kampeni hii, pamoja na mabalozi wetu wakuu: Mtangazaji wa Runinga Floortje Dessing na mwana anga André Kuipers.

Kupitia msaada mzuri wa aina yetu wa washirika wetu wa vyombo vya habari, tulizindua kampeni nchi nzima, kupitia mabango, runinga za kidigitali redio na runinga, vyombo vya Habari vya kijamii, sinema, na matangazo ya kidigitali.

 

Kuleta suluhisho kwa mabadiliko ya hali ya hewa
Tangu tulipoanza nchini Uholanzi, kampeni zetu zimebadilika kabisa. Hapo mwanzo, sote tulikuwa tukieneza juu ya matazimio yetu. Sasa tunaweza kuonyesha mafanikio yetu ya kukijanisha na faida ya njia yetu ya  asili. Lengo letu pekee ni kueneza ujumbe huu mzuri, kuwafanya watu wafahamu na kuwaletea matumaini: kuna suluhisho la mabadiliko ya hali ya hewa.

Shukrani kwa washirika wetu wazuri tumeweza kufikia mamilioni ya watu na tumepokea mamilioni ya fedha ya sarafu ya ulaya katika kudhamini vyombo vya Habari. Harakati zimeanza

MATOKEO TUNAYOJIVUNIA

12 + million

Watu million kumi na mbili wamefikiwa na kampeni zetu za utayari

HAMASISHA, UNGANISHA NA AMSHA

Ikiwa unataka kufanya mabadiliko ya ulimwengu, unahitaji kuwa kila mahali: habari, matangazo, vituo vya kijamii, mazungumzo, na zaidi ya yote katika mioyo na akili za watu. Ili kufanya hivyo, tunatumia nguvu ya vyombo vya habari na mawasiliano, kujenga utayari na uelewa na kuonyesha kuwa kwa pamoja tunaweza kuwa na athari chanya na muhimu kwa mabadiliko ya hali ya hewa.

Kampeni zetu za kimataifa za uelimishaji mtandaoni na nje ya mtandao zinatengenezwa ili kukuza njia za asili na kuhamasisha, kuunganisha na kuamsha kizazi kizima na kukuza harakati za kurudisha mazingira.

0(option 2)_header_farmers spread the word_dig in_Justdiggit_Kisiki Hai__roadshow_2018_marchaers_Dodoma_Tanzania

Kampeni za uholanzi

  • 2022/2023
  • 2021
  • 2019/2020
  • 2018
  • 2017
  • 2016
  • 2013
  • Shughuli zingine za kampeni za Uholanzi

Kampeni 2022/2023

Ni rahisi kuamini katika kurejesha kijani wakati unaweza kuona kwa macho yako kwamba inafanya kazi. Ndiyo maana hivi majuzi tulizindua kampeni yetu mpya ya ‘The greener, the cooler’, pamoja na mshirika wetu wa muda mrefu, wakala wa ubunifu, Havas Lemz. Jitayarishe kusafirishwa hadi Afrika!

poster

Kampeni 2021

Miaka 10 iliyobaki kuchukua hatua inamaanisha wakati wa kuharakisha na kuongeza ukuaji wa kukijanisha Afrika! Katika kampeni yetu mpya, tunakaribisha kila mtu kuwa sehemu ya mabadiliko na kujiunga nasi katika malengo yetu ya kuupoza ulimwengu CHIMBA!

poster

Kampeni 2019/2020

Ili kukuza njia yetu ulimwenguni, tunaendeleza kampeni chanya. Kampeni yetu ya 2019/2020 inaelezea jinsi miradi yetu ya kukijanisha inavyofanya kazi na inaonyesha matokeo katika muda wa miezi michache tu. Chimba | Kijani | Baridi, ni rahisi sana.

poster

Kampeni 2018

Kampeni yetu ya 2018 inaonyesha matokeo mazuri ya miradi yetu nchini Kenya na jinsi njia yetu inavyofanya kazi. Ujumbe ambao tunataka kuwashirikisha ni kwamba kukijanisha kwa kiwango kikubwa sio tu una athari chanya kwa hali ya hewa, pia inachangia moja kwa moja kwa usalama wa maji na chakula, bioanuwai, na kukuza uchumi wa eneo.

Kampeni hiyo inapatikana tu kwa Uholanzi.

poster

Kampeni 2017

Kampeni ya Justdiggit ya 2017 inaonyesha kazi yetu na matokeo ya moja ya miradi yetu nchini Kenya. Inaonyesha na picha halisi tofauti ya kijani kibichi baada ya miezi 8 tu, kutoka  ardhi kavu hadi kijani kibichi na yenye rutuba.

Kampeni hiyo inapatikana tu kwa Uholanzi.

poster

Kampeni 2016

Kampeni ya 2016 iliunganisha koleo la kijani na miradi ambayo tunaendelea nayo na kuipasha dunia na Malengo mengine ya Maendeleo Endelevu.

Biashara hiyo inasimuliwa na balozi wa kiholanzi Astronaut André Kuipers

poster

Kampeni 2013

Kampeni yetu ya kwanza ilimshirikisha Askofu Mkuu Desmond Tutu: mwanaharakati wa haki za binadamu wa Afrika Kusini. Kwa juhudi zake dhidi ya ubaguzi wa rangi, alipokea Tuzo ya Amani ya Nobel. Yeye ndiye mlezi na balozi asiyechoka wa Justdiggit.

poster

Shughuli zingine za kampeni za Uholanzi

Tukio: Mradi wa Raindance
Kwa kuwa hakuna harakati bila muziki, tulizindua Mradi wa Raindance: mfululizo wa matamasha ya moja kwa moja ya miaka miwili, kusherehekea na kuonyesha uwezekano wa kuongoa mazingira ulimwenguni – na kutafuta fedha kwa miradi yetu barani Afrika. Tamasha hilo lilifanyika wakati huo huo katika maeneo matatu tofauti (Kenya, Tanzania, na Uholanzi), na maeneo yote yalikuwa ya moja kwa moja yakiunganishwa, ili kuleta pamoja harakati moja na kusherehekea kujipanga tena pamoja.

Kwa sababu ya COVID-19, tulilazimishwa  kulisitisha tamasha la Raindance hadi taarifa nyingine zitakapotoka

Kuelimisha watoto na Meester Boy
Wanafunzi wa shule za msingi ndio kizazi cha kwanza kukabiliwa kweli na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na kizazi hiko kufanya kitu juu yake.

Meester Boy hufundisha watoto juu ya umuhimu wa hewa ya kaboni, udongo, maji, bioanuwai, na suluhisho la Justdiggit kwa mabadiliko ya hali ya hewa. Kwa maarifa haya, tunatarajia kuhamasisha na kuwatia moyo watoto kuwa sehemu ya mapinduzi ya kijani kibichi!

Safari ya watu wenye ushawishi kwenda Tanzania na Kenya
Tunafanya kazi pamoja na washawishi wa kijamii, tukiwafikia walengwa wapya, walengwa wachanga, kushiriki kazi zetu na umuhimu wa kukijanisha

Katika 2019 tuliungana na Wakala wa Uuzaji wa Ushawishi (IMA). Pamoja nao, tuliandaa safari na washawishi kutembelea miradi yetu nchini Kenya na Tanzania, ambapo walionyesha ulimwengu uwezo wa kukijanisha. Hii ilisababisha ongezeko kubwa la ufuasi kwenye mitandao yetu ya kijamii

NJIA YETU

Jinsi tunavyoendesha kampeni za uhamasishaji

Ikiwa unataka kuanza harakati, unahitaji kuwa kila mahali: habari, matangazo, yaliyomo, vituo vya kijamii, mazungumzo, na zaidi ya yote katika mioyo na akili za watu. Justdiggit hutumia nguvu za kila aina ya njia za vyombo vya habari na mawasiliano ili kufanya hivyo; kuunda ufahamu, uelewa na kuleta suluhisho la mabadiliko ya hali ya hewa, yote kwa mtazamo mzuri.

Kampeni zetu za uhamasishaji za nje na nje ya mtandao ni sehemu ya mkakati wetu mkubwa wa mawasiliano na umeendelezwa kukuza suluhisho za asili na kuhamasisha, kuunganisha na kuamsha kizazi kizima na kukuza harakati za kurudisha mazingira.

WASHIRIKA

Washirika wetu ndani ya uholanzi

Washirika wetu wote
andre kuipers out of home

Mabalozi

Tunafanya kazi Pamoja na watu mashuhuri kadhaa ndani  ya uholanzi kusambaza ujumbe wetu.

KAZI ZINGINE

Kazi zetu zote