Privacy Statement
Tunaamini kuwa faragha yako ni muhimu sana, na kwa hivyo tunashughulikia data yako ya kibinafsi kwa uangalifu mkubwa. Katika taarifa ya faragha iliyo hapa chini tunaeleza hili kwa undani zaidi na kufafanua ni kanuni zipi tunazofuata.
Privacy Statement
Justdiggit huchakata data ya kibinafsi na data nyingine kwa mujibu wa sheria ya faragha: Kanuni ya Jumla ya Ulinzi wa Data (GDPR).
1. Utangulizi
Stichting Justdiggit Foundation (“Justdiggit”, “sisi”, “yetu”), iliyoko Prins Hendrikkade 25, 1012 TM Amsterdam, Uholanzi, inafanya kazi kama mdhibiti wa data kwa ajili ya uchakataji wa data binafsi ulioelezwa katika Sera hii ya Faragha. Data binafsi ni taarifa yoyote inayoweza kumtambua mtu wa asili (moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja).
Tumejizatiti kushughulikia data binafsi kwa uangalifu na kwa mujibu wa Kanuni ya Jumla ya Ulinzi wa Data (GDPR) pamoja na sheria za ndani zinazotumika katika nchi tunazofanya kazi, ikiwemo Uingereza, Tanzania na Kenya.
2. Tunakusanya data gani binafsi na kwa nini?
Justdiggit hukusanya data zako binafsi unapotumia huduma zetu na/au unapozitoa kwetu mwenyewe. Tunakusanya taarifa binafsi kutoka kwa:
- Wafadhili (watu binafsi na mashirika);
- Washiriki wa programu (kwa mfano wakulima, vikundi vya jamii, viongozi wa maeneo);
- Washirika (vyombo vya habari, taasisi za utafiti, taasisi mbalimbali, biashara, wakfu na wafadhili);
- Watumiaji wa tovuti;
- Wakandarasi na watoa huduma;
- Wafanyakazi wa mashirika washirika;
- Wajumbe wa Bodi ya Usimamizi;
- Washirika watarajiwa na watu wanaoweza kushirikiana nasi.
Hapo chini tunaeleza, kwa kila msingi wa kisheria, ni data gani binafsi tunachakata na kwa madhumuni gani.
UTEKELZAJI WA MKATABA NA MASLAHI HALALI
Pale ambapo wewe ni upande katika mkataba nasi—kama mfadhili, mshiriki wa programu, mshirika, mkandarasi, mtoa huduma, mjumbe wa Bodi ya Usimamizi au mshirika mtarajiwa—tunachakata data zako binafsi kwa msingi wa utekelezaji wa mkataba. Pale ambapo uchakataji unahusu watu ambao si wahusika wa moja kwa moja wa mkataba (kama wafanyakazi wa mashirika washirika), tunategemea maslahi yetu halali, kwa kuwa hatuwezi kutoa huduma zetu, kutekeleza na kufuatilia programu zetu au kuwasiliana na wafadhili, washirika na wadau bila data hiyo.
Kulingana na uhusiano wako nasi, data binafsi tunazochakata kwa misingi hii zinaweza kujumuisha: taarifa za mawasiliano (jina, barua pepe, namba ya simu, anwani, shirika), taarifa za utambulisho (mahali na tarehe ya kuzaliwa, jinsia, picha), taarifa za kifedha (michango, historia ya malipo, taarifa za benki), taarifa za malipo (marejeo ya miamala), taarifa za mawasiliano (barua pepe na historia ya mawasiliano), taarifa za programu (ushiriki, mahudhurio, taarifa za kaya au kijiji, eneo la kijiografia inapofaa), taarifa za kitaaluma (cheo cha kazi, shirika, maelezo ya mkataba) na taarifa za kiufundi.
WAJIBU WA KISHERIA
Justdiggit huchakata data binafsi kama vile taarifa za mawasiliano, taarifa za utambulisho, taarifa za kifedha na taarifa za malipo kwa msingi wa wajibu wa kisheria, kwa mfano kuhusiana na wajibu wetu wa kodi.
RIDHAA
Justdiggit huchakata data binafsi kama vile taarifa za mawasiliano, taarifa za kiufundi (anwani ya IP, kivinjari, kifaa, vidakuzi) na taarifa za programu (picha na video za washiriki wa programu) kwa msingi wa ridhaa yako. Tunafanya hivyo ili kutuma majarida, taarifa za kampeni, pamoja na kwa madhumuni ya uchapishaji na mawasiliano. Pia tunachakata taarifa zako za mawasiliano kwa msingi wa ridhaa ili kukupa taarifa kuhusu chaguzi za kuchangia, ikiwemo michango ya mara kwa mara na wasia wa mali.
Unaweza kuondoa ridhaa yako wakati wowote kwa kutumia kiungo cha kujiondoa kilicho chini ya kila jarida au kwa kuwasiliana nasi kupitia info@justdiggit.org. Kuondoa ridhaa yako hakuathiri uhalali wa uchakataji uliofanyika kabla ya kuondolewa kwa ridhaa hiyo.
3. Uhifadhi wa Data
Tunahifadhi data binafsi kwa muda unaohitajika tu kwa madhumuni yaliyoelezwa katika Sera hii ya Faragha na kwa ajili ya kutimiza mahitaji yoyote ya kisheria, kihasibu au ya utoaji taarifa.
Pia kuna aina fulani za taarifa, kama vile rekodi za kodi, ambazo sheria zinahitaji zihifadhiwe kwa kipindi maalum. Tutafuta data zako binafsi ikiwa hatuzihitaji tena kwa madhumuni hayo.
Katika baadhi ya mazingira tunaweza kufanya taarifa zako binafsi zisiweze kukutambulisha (anonymisation), na katika hali hiyo tunaweza kutumia taarifa hizo bila kukupa taarifa zaidi.
Vipindi maalum vya uhifadhi vimeainishwa ndani ya Rekodi yetu ya Shughuli za Uchakataji (ROPA). Ikiwa una maswali kuhusu vipindi vya uhifadhi, tafadhali wasiliana nasi kupitia privacy@justdiggit.org.
4. Kushiriki Data Binafsi
Hatuuzi data zako binafsi. Tunashiriki data binafsi pale tu inapohitajika kwa utekelezaji wa makubaliano, kufuata wajibu wa kisheria na/au kulinda maslahi halali ya shirika.
Tunaweza kushiriki data na:
- Watoa huduma (wachakataji wa data), ikiwemo watoa huduma za malipo, majukwaa ya mawasiliano na watoa huduma za TEHAMA;
- Washirika wa teknolojia kama Microsoft na Google;
- Watoa huduma za TEHAMA na usalama, ikiwemo QNP na Eye Security;
- Washirika wa programu wanaoshiriki katika utekelezaji wa miradi;
- Mamlaka husika pale sheria inapohitaji;
- Taasisi za ndani ya kundi la Justdiggit, ikiwemo mashirika ya Justdiggit nchini Kenya, Tanzania, Senegal na Uingereza, pale inapohitajika kwa uratibu wa shughuli, utekelezaji wa programu na utoaji wa taarifa.
Tunakikisha mikataba inayofaa ya uchakataji wa data ipo kati yetu na wahusika wote husika.
5. Uhamishaji wa Data Kimataifa
Kama shirika la kimataifa, baadhi ya data binafsi zinaweza kuchakatwa nje ya Eneo la Kiuchumi la Ulaya (EEA), ikiwemo katika nchi kama Marekani na Kenya.
Pale data binafsi zinapohamishwa nje ya EEA, tunahakikisha kuwa hatua stahiki za ulinzi zimewekwa, kama vile:
- Vifungu vya Kawaida vya Mikataba (Standard Contractual Clauses – SCCs) vilivyoidhinishwa na Tume ya Ulaya;
- Hatua za ziada za kiufundi na kiutawala inapohitajika;
- Uhamishaji kwenda katika nchi zilizoidhinishwa kuwa na kiwango cha kutosha cha ulinzi wa data pale inapofaa.
Hatua hizi zinahakikisha kuwa data zako binafsi zinaendelea kulindwa kwa mujibu wa GDPR.
6. Vidakuzi (Cookies) na Teknolojia za Ufuatiliaji
Tunatumia vidakuzi na teknolojia zinazofanana ili kuhakikisha tovuti yetu inafanya kazi ipasavyo na kuboresha uzoefu wa mtumiaji.
Tunatumia:
- Vidakuzi muhimu;
- Vidakuzi vya mapendeleo;
- Vidakuzi vya uchambuzi;
- Vidakuzi vya masoko (kwa ridhaa yako pekee).
Pale inapohitajika, tunaomba ridhaa yako kabla ya kuweka vidakuzi visivyo muhimu. Unaweza kudhibiti au kuzima vidakuzi kupitia mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali soma Sera yetu ya Vidakuzi.
7. Usalama wa Data
Tunatumia hatua zinazofaa za kiufundi na kiutawala kulinda data binafsi, ikiwemo udhibiti wa ufikiaji, usimamizi wa vifaa na akaunti, ufuatiliaji wa usalama wa mifumo, usimbaji wa data, masasisho ya programu, utambuzi wa matukio ya usalama na mafunzo ya wafanyakazi kuhusu usiri wa taarifa.
8. Haki Zako
Kwa mujibu wa GDPR, una haki ya:
- Kufikia data zako binafsi;
- Kusahihisha data zisizo sahihi;
- Kuomba kufutwa kwa data (“haki ya kusahaulika”);
- Kuzuia uchakataji;
- Kupinga uchakataji;
- Kuhamisha data;
- Kuondoa ridhaa yako wakati wowote.
Haki hizi si za moja kwa moja katika kila hali. Unaweza kutumia haki zako kwa kuwasiliana nasi kupitia privacy@justdiggit.org. Tutashughulikia ombi lako kwa mujibu wa GDPR na kukujulisha hatua zilizochukuliwa ndani ya mwezi mmoja tangu kupokea ombi lako. Kipindi hiki kinaweza kuongezwa kwa miezi miwili kutokana na ugumu wa ombi au wingi wa maombi tunayopokea.
9. Malalamiko
Una haki ya kuwasilisha malalamiko kwa mamlaka ya usimamizi ya Uholanzi, Autoriteit Persoonsgegevens, au mamlaka husika katika eneo lako. Orodha ya mamlaka ya usimamizi ya Umoja wa Ulaya na maelezo yao ya mawasiliano yanapatikana hapa.
10. Maelezo ya Mawasiliano
Kwa maswali kuhusu Sera hii ya Faragha au ulinzi wa data, wasiliana nasi kupitia: privacy@justdiggit.org