Shirika la Justdiggit lazindua app ya Kijani ili kuongeza kasi ya ukijanishaji kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika
ANGALIA NA UJIFUNZE
Waongozaji wazuri wa filamu vijana wamekuwa wakifanya kazi nasi kufanikisha hii. Katika filamu na majarida yetu tunaonyesha njia yetu ya kurudisha asili, na matokeo ya kuvutia suluhisho rahisi la kukijanisha. Tazama sinema zetu hapa:
Kwa vizazi vingi, watu wa Samburu na mifugo wao wamekuwa na uhusiano wa kina na maji, kulingana na mvua kwa maisha yao.
Wanaume wanachimba visima vya kuimba; wanawake wanachota maji huku wakiimba na kuomba mvua. Kati ya 2020 na 2023, Kenya ilikumbwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 40. Mvua ilikaa, visima vilikauka, na ng’ombe na wanyamapori walikufa. ‘The Land Smiles Back’ ni hadithi ya jamii ya Wasamburu katika Hifadhi ya Westgate, ambao walifanya ardhi itabasamu tena kwa kurejea katika teknolojia ya zamani ya maji.
‘The Land Smiles Back’ imetayarishwa kwa pamoja na Justdiggit, The Safari Collection, na jumuiya ya Samburu ya Westgate Community Conservancy. Filamu ilishinda nafasi ya kwanza, kati ya mawasilisho 131 kutoka nchi 45 tofauti, kwenye Tuzo la Filamu ya Maji ya 2025. Tamasha hili fupi la filamu limeandaliwa na ‘Tuzungumze Kuhusu Maji’ kwa ushirikiano na UNESCO Intergovernmental Hydrological Programme, Mtandao wa Kimataifa wa Makavazi ya Maji, Water As Leverage, CeReGAS, na Kongamano la 1 la Maji la Amerika Kusini.
Ndani ya mfululizo huu watu kadhaa waliohusika katika mradi wa kurejesha kijani kibichi huko Monduli, Tanzania wanashiriki uzoefu wao binafsi katika mfululizo wa mahojiano.
Katika kipindi hiki cha pili tunapata kujua utoto, matumaini na matakwa ya watu wanne waliohusika katika mradi huo.
Jarida hili fupi la Justdigit linaonyesha miradi inayoendelea, kuchimba makinga maji ya nusu mwezi 72.000 kwa ajili ya kuvuna maji ya mvua na kurejesha ardhi iliyo haribika.
Mfuatano wa tuzo za ushindi za jarida la utengenezaji wa mvua. Ambapo utengenezaji wa mvua una onyesha kuanza kwa miradi ya Just dig it na umuhimu wake, mbegu ya mabadiliko inaonyesha hatua tulizopiga na jinsi gani kukijanisha kuna faidisha sisi sote.
Utengenezaji wa mvua III unaeleza hadithi kuhusu kusambaza mawazo ambayo yanaweza kurudisha mamilioni ya miti kurudi hali ya uhai. Kisiki Hai! Ujumbe wa matumaini na chanya. Inaonyesha faida chanya za miti katika namna tofauti. Unataka kujua kuhusu hizi faida? Angalia jarida letu!
Hamasika!
Ndani ya sinema hii ya elimu unajifunza yote juu ya athari chanya za Kisiki Hai. Yona, mkulima anayeishi mkoa wa Dodoma, anamtembelea mkulima Augustino, ambaye anatekeleza njia ya Kisiki Hai kwenye shamba lake kwa miaka mingi. Yona anagundua kuwa kurudisha miti kwenye ardhi yako kunaweza kuifanya ardhi yako kuwa ya kijani na yenye rutuba tena, na kuifanya iwe rahisi sana kukuza mazao. Unataka kujua jinsi ardhi iliyojaa miti inaweza kuonekana? Tazama sinema ya Kisiki Hai I!
Hamasika!
Ndani ya Kisiki Hai II unajifunza hatua nne tofauti za Kisiki Hai, inayokuwezesha kuitumia kwenye ardhi yako mwenyewe. Unajifunza msaada wa kumbukumbu, ukihakikisha unaweza kukumbuka hatua zote kwa urahisi. Mbinu mpya ya kukijanisha miti huletwa pia, Fanya Juu na Fanya Chini, ikikusaidia kuvuna maji ya mvua yanayoanguka kwenye ardhi yako. Hii inaongeza upatikanaji wa maji kwa mazao, kuhakikisha inaweza kukua vizuri. Tazama sinema hii ya elimu na uanze mwenyewe!