SABABU NA MATOKEO

Nini kinasababisha ukame katika ardhi?
Ni yapi matokeo ya ardhi kuwa kavu?

NINI KINASABABISHA UKAME
KATIKA ARDHI?

Kwa sababu ya ongezeko la idadi ya watu ulimwenguni tunahitaji zaidi na zaidi kutoka kwenye ulimwengu, kwa kweli tunahitaji zaidi kwenye ardhi kubwa.

Hii inaitwa utumiaji kupita kiasi. Inasababisha kupungua kwa ardhi, kupunguzwa kwa udongo wenye rutuba na kukausha  ardhi. Hasa katika maeneo hatarishi, ambapo maji na udongo wenye rutuba  unahatarishwa, matokeo ya uvunaji kupita kiasi  huhisiwa kila siku. Mfano ni eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika. Mabadiliko ya hali ya hewa katika maeneo haya yanazidi kusababisha vipindi vya ukame na joto kali. Mvua inapofika, mara nyingi huwa kubwa sana. Kwa sababu maji mengi yanashuka mara moja, maji hayana wakati wa kupenya kwenye udongo. Kwa kuongezea, kukata miti kwa  ajili ya kuni, malisho kupita kiasi ya maeneo yenye nyasi na mazoea yasiyofaa ya matumizi ya ardhi kunasababisha kupungua kwa mimea. Ardhi inakuwa wazi na haina kinga, na kuongeza ukame wa ardhi.

Climate change CO2 emissions Chimney Justdiggit

NI YAPI MATOKEO YA
ARDHI KUWA KAVU?

Kukauka kwa ardhi kunasababisha jangwa na maeneo makubwa ya ardhi iliyoharibika.

Hii inamaanisha ni ngumu kupata chakula, mazao, maji safi na maliasili kama kuni kutoka ardhini. Mbali na hayo, ukosefu wa mvua husababisha kutopatikana kwa mazao. Mvua inapofika, ni kwa muda mfupi na kubwa, bila kuacha nafasi ya kuweza kupenya kwenye udongo. Maji yanafurika kwa maeneo yenye miteremko, yakiondoa tabaka la juu la udongo wenye rutuba, pia huitwa mmomonyoko. Kwa sababu ya kuondoa  udongo  wenye rutuba na kupungua kwa maji kwenye udongo, ni ngumu kukuza mazao, na kusababisha uhaba wa chakula kwa jamii za wenyeji. Mwishowe inaweza kusababisha umasikini na njaa ndani ya maeneo haya. Ukame hauathiri tu wanadamu, pia mimea na wanyama wanakabiliwa na matokeo ya ukame. Kwa sababu ya ukame, mimea michache inaweza  kukua, na bioanuwai ya mimea na wanyama inapungua.

Climate change - drought in Africa - Justdiggit
Temperature difference vegetation soil

TUNAWEZA KUFANYA NINI KUHUSU HILI?

Kukijanisha husaidia! Mimea huendeleza ufyonzwaji wa kaboni, baridi ya udongo, na huchochea mzunguko wa maji. Maji huvukizwa nje ya matundu ya mimea na miti, na kuongeza unyevu. Uundaji wa mawingu huchochewa na mvua huongezeka. Mizizi ya mimea husaidia maji kupenya kwenye udongo. Kwa kuongezea, mizizi hii husaidia kuhifadhi safu ya juu yenye rutuba ya udongo wakati wa mvua kubwa, kuzuia mmomonyoko wa udongo wenye rutuba. Ardhi inaweza kutumika kwa kilimo tena, ikiongeza usalama wa chakula na mapato kwa watu na kupanua bioanuwai.

NI NANI HAO Justdiggit?

Na Jinsi gani Justdiggit wanasaidia kupambana na kutoa gesi ya kaboni na kupoooza sayari?

Justdiggit ni shirika la Uholanzi likiwa na lengo la kurejesha mifumo ya mazingira iliyoharibika kwa kukuza, kuanzisha na kufadhili mipango mikubwa ya urejesho wa mazingira ndani ya Afrika. Miradi yetu ya kukijanisha husaidia kurejesha ulinganifu wa maji kwenye udongo na kurudisha mimea, ambayo ina athari nzuri kwa hali ya hewa ya eneo , inaongeza usalama wa maji na chakula na inakuza bioanuwai ndani ya maeneo ya mradi. Ndani ya miradi yetu tunafanya kazi pamoja na washirika wa ndani na jamii. Jamii zilizohusika moja kwa moja zinanufaika na programu zetu tunapounda mazingira bora ya kuishi na kuongeza maendeleo ya uchumi. Njia yetu ya kipekee ni mkakati wa vyombo vya habari na mawasiliano, unaojumuisha mawasiliano na vyombo vyote vya habari vinavyopatikana kwa kiwango cha mitaa, mkoa, kitaifa na kimataifa. Pamoja na kampeni hizi za vyombo vya habari zilizodhaminiwa, tunakusudia kukuza athari ya programu za urejesho wa mazingira, na hivyo kuunda harakati za kurudisha mazingira, na kukuza kukijanisha barani Afrika.

poster