Miradi ya kukijanisha
Amboseli & Olgulului-Ololarashi, Kenya
Kurejesha mfumo wa ekolojia katika maeneo ya machungio Kaskazini mwa Kenya
Kwa kushirikiana na washirika wetu katika utekelezaji, tunarejesha uoto endelevu katika maeneo husika kwa kutumia na kuhamasisha matumizi ya mbinu bora za utunzaji wa malisho. Kuna mbinu muhimu mbili ambazo ni uanzishaji wa makingamaji ya nusu duara ya kuvunia maji na uanzishaji wa hifadhi za mbegu za nyasi.
Eneo la Kaskazini mwa Kenya linajumuisha kaunti (majimbo) za Laikipia, Isiolo, Samburu na Marsabit. Eneo hili limegawanyika katika hifadhi kadhaa za kijamii zinazounganisha mifumo muhimu ya ekolojia na hifadhi, jambo lenye mchango mkubwa katika jitihada za uhifadhi za kanda hii. Kimsingi, hifadhi hizi ni makazi ya jamii za kifugaji zinazotegemea ufugaji wa wanyama kama shughuli yao ya pekee ya kuendeshea maisha yao. Eneo la Kaskazini pia linatumika kama njia muhimu ya makundi makubwa ya wanyama pori yanayohama kwenda nchi mbalimbali.
Suala la usimamizi mzuri wa machungio bado linabaki kuwa ni changamoto kubwa katika eneo hili, linahitaji mbinu shirikishi badala ya kutumia mbinu moja kama suluhisho pekee. Ili kutatua hili, tumeunganisha nguvu na washirika mbalimbali, ikiwa ni pamoja na washirika wenyeji kama vile Northern Rangelands Trust (NRT), hifadhi za kijamii, Green Earth Warriors, Wyss Academy of Nature na wengine wengi ili kuimarisha na kuboresha ardhi hii iliyoharibiwa pamoja na nyika kwa njia ya usimamizi mzuri.
Matokeo ya jitihada hizi kwa pamoja yanachangia kuziwezesha jamii kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira.
Hekta za ardhi zinazoendelea kuboreshwa
Matuta ya kuvunia maji yamechimbwa
Hifadhi za mbegu za nyasi
Watu wananufaika
Kwa kushirikiana na wakulima na wafugaji, tunaboresha maelfu ya hekta za ardhi kame na iliyoharibiwa katika eneo la Laikipia, Isiolo, Samburu na Marsabit, upande wa nyanda za kaskazini. Urejeshaji wa uoto umekuwa na matokeo mengi chanya katika tabianchi, mazingira na bayoanuwai, kwa watu na maisha yao kwa ujumla.
Matuta ya kuvunia maji (au kama tunavyopenda kuyaita: “tabasamu la dunia”) ni makingamaji yenye umbo la nusu duara ambayo hutumika kuvunia maji ya mvua.
Matuta haya yanachimbwa katika maeneo mbalimbali ya mradi barani Afrika ili kuvuna maji ya mvua ambayo vinginevyo yangetiririka na kupotea katika ardhi kame na tupu. Kwa kuchimba matuta ya kuvunia maji, tunaweza kukijanisha eneo kubwa zaidi kwa muda mfupi, na kunufaisha bayoanuwai, uoto, watu na – hatimaye tabianchi yetu.
Emurua, Arusha Mei 2023.
Katika hifadhi zetu za mbegu za nyasi, wanawake wanapanda, wanavuna na wanauza nyasi (nyasi kavu) na mbegu. Wanajipatia kipato kwa kuziuza kwenye masoko yao au katika mashirika. Hifadhi za mbegu za nyasi hutengeneza kichaka cha kijani jangwani, na nyasi kavu wanayoyavuna akina mama hutumika kama chakula cha mifugo yao nyakati za ukame.
Uuzaji wa nyasi na mbegu za nyasi zilizovunwa kutoka kwenye hifadhi za mbegu za nyasi huwatengenezea kipato wanawake wanaotunza hifadhi hizo. Kipato hiki hutumika kama mbadala wa kuendesha maisha, na kuwafanya wanawake wasiwe tegemezi.
Jumla ya wanawake 150 wanajihusisha na hifadhi hizi za mbegu za nyasi.
Kuwezesha watu, mmoja baada ya mwingine, katika kukijanisha ardhi yao ni mbinu yenye gharama nafuu, mbinu madhubuti na ni kichocheo cha mabadiliko ya kijamii na kiuchumi. Ili kutimiza jambo hili, tunahitaji kufahamika kwa watu. Hivyo, tunahamasisha wakulima kwa kuwaonesha faida za kuboresha ardhi sambamba na kuwapa mbinu za jinsi ya kuanza.
Wakulima katika mazingira ya Kaskazini, Kenya. Na: Nick Spolin
Matuta ya kuvunia maji ni makingamaji ya nusu duara yanayotengenezwa kwa ajili ya kufunua tabaka gumu la juu la udongo.
Matuta haya hupunguza kasi ya maji na hutumika kuvuna maji yanayotiririka kutoka milimani, na kuzuia mmomonyoko wa udongo wenye rutuba. Pia, hurejesha mlinganyo wa maji katika udongo, hali inayoongeza upatikanaji wa maji kwa ajili ya mbegu ambazo bado zipo ardhini. Mbegu hizi sasa zinapata nafasi ya kuota, yaani: ukijanishaji! Katika Mradi wa Mazingira wa eneo la Kaskazini, jamii ya Kimasai tayari imeshachimba zaidi ya matuta 100,000 ya kuvunia maji!
Fanya Juu na Fanya Chini ni mbinu zinazotumika kuvunia maji ya mvua. Wakulima huchimba makinga maji katika mashamba yao ili kuzuia mmomonyoko na kuvuna maji ya mvua ambayo ni muhimu katika ardhi zao.
Fanya Chini maana yake ni ‘tupa udongo upande wa chini’. Hii huzuia maji ya mvua kutoka nje ya shamba kuingia shambani, jambo linalozuia mmomonyoko wa udongo wenye rutuba. Fanya Juu inamaanisha ‘tupa udongo upande wa juu’, huzuia maji ya mvua katika shamba yasitoke shambani, jambo linaloongeza upatikanaji wa maji kwa ajili ya mazao. Mwishowe, huwasaidia wakulima kukijanisha zaidi mashamba yao!
Hifadhi za mbegu za nyasi ni sehemu ndogo ya ardhi ya jamii ambayo hutumika katika uzalishaji wa nyasi na mbegu za nyasi.
Hifadhi za mbegu za nyasi zinasimamiwa na kuhudumiwa na vikundi vya wanawake wa Kimasai. Nyasi zikikomaa vizuri, nyasi hizo hutoa mbegu ambazo huuzwa na wanawake kwenye masoko yao au katika miradi mingine ya ukijanishaji. Hii husaidia kuongezeka kwa pato la wanawake pamoja na kijani kibichi katika maeneo mengine, jambo lenye faida kwa pande zote mbili!
Ili kuhakikisha miradi inakuwa endelevu, tutaanzisha mpango wa usimamizi wa malisho kwa kushirikiana na washirika wetu waliopo katika maeneo husika pamoja na jamii.
Lengo ni kuzuia ufugaji wa mifugo mingi kupita kiasi katika maeneo yaliyoharibiwa na yale yaliyo katika hatari ya kuharibiwa.
Ili kuona kuona kutatua jinsi suluhisho zinazotegemea asili zinavyobadilisha, kanuni za ikolojia, na maisha ya jamii kwa ujumla, ni muhimu macho yako mwenyewe.
Lakini hapo ndipo changamoto inapoanza: hatuwezi kuleta watu wote duniani kwenye miradi yetu. maana tumeunda suluhisho hili la kupita kupitia uzoefu wa mwingiliano. Tumefanya maajabu ya miradi yetu ya kijani kibichi yaweze kufika moja kwa moja kwako—popote ulipo!
Ingia sasa na ujionee uzuri wa shamba la matuta ya kuvunia maji na hifadhi za mbegu za nyasi kwa macho yako mwenyewe.
Tuko kwenye dhamira ya kuhamasisha mamilioni ya watu kuchukua hatua kurekebisha hali ya kijani kibichi katika Afrika
Ikiwa tunataka kupooza sayari kwa muongo mmoja, kila mtu anahitaji kuwa kwenye mabadiliko. Kupitia nguvu ya vyombo vya habari, mawasiliano, taarifa, na teknolojia ya kisasa tunaweza kueneza ujumbe wetu na kuongeza kiwango. Tunataka kuhamasisha, kuunganisha na kuwezesha kizazi kizima, kukuza harakati za kurudisha mazingira.