Kuongeza ustahimilivu wa kilimo na ufugaji kupitia uboreshaji wa ardhi

Kwa kushirikiana na washirika wetu katika utekelezaji, tunarejesha uoto endelevu katika maeneo husika kwa kutumia na kuhamisha mbinu bora na zenye tija za usimamizi. Kuna mbinu mbili muhimu ambazo ni uanzishaji wa makingamaji ya kuvunia maji ya nusu duara na uanzishaji wa hifadhi za mbegu za nyasi.

Eneo la katikati ya Tana nchini Kenya linajumuisha kaunti (majimbo) za Kitui, Machakos, Makueni, Tharaka Nithi na Tana River maeneo yaliyo katika ukanda wenye ardhi kame katika eneo la Mashariki ya Chini nchini Kenya. Eneo hili linajumuisha ardhi ya kilimo na ufugaji inayomilikiwa na wakulima huku ikiunganisha mifumo ya ekolojia na hifadhi, ambayo ni muhimu katika jitihada za uhifadhi za kikanda. 

Usimamizi endelevu wa ardhi unabaki kuwa changamoto kubwa ndani ya maeneo haya, jambo linalohitaji mbinu shirikishi badala ya kutegemea mbinu moja kama suluhisho pekee. Ili kukabiliana na hili, tumeshirikiana na wadau muhimu, ikiwa ni pamoja na Anglican Development Services Eastern, viongozi wa maeneo husika, serikali za majimbo, na jamii ili kuimarisha na kuboresha ardhi hii iliyoharibiwa, kwa njia ya usimamizi mzuri. Matokeo ya juhudi hizi kwa pamoja huchangia katika ustahimilivu wa jamii dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira. Vilevile, hii imesababisha wakulima kuiga mbinu mpya za ukijanishaji katika mashamba ya watu binafsi.

Tumefanikiwa katika Eneo la katikati ya Tanai mpaka sasa

500 Hekta

za ardhi zinazoendelea kuboreshwa

50.000

Matuta ya kuvunia maji yamechimbwa

5

Hifadhi za mbegu za nyasi

>10.000

Watu wananufaika

Tunaboresha maelfu 500 ya hekta za ardhi

Kwa kushirikiana na wakulima na wafugaji, tunaboresha maelfu ya hekta za ardhi kame na iliyoharibiwa katika eneo la Makueni, Kitui and Machakos. Urejeshaji wa uoto umekuwa na matokeo mengi chanya katika tabianchi, mazingira na bayoanuwai, kwa watu na maisha yao kwa ujumla.

1 JustDiggit-Schep, campagne 2017 - better shovel - 1920x1080-2576

Tumechimba matuta ya kuvunia maji zaidi ya elfu 50

Matuta ya kuvunia maji (au kama tunavyopenda kuyaita: “tabasamu la dunia”) ni makingamaji yenye umbo la nusu duara ambayo hutumika kuvunia maji ya mvua. 

Matuta haya yanachimbwa katika maeneo mbalimbali ya mradi barani Afrika ili kuvuna maji ya mvua ambayo vinginevyo yangetiririka na kupotea katika ardhi kame na tupu. Kwa kuchimba matuta ya kuvunia maji, tunaweza kukijanisha eneo kubwa zaidi kwa muda mfupi, na kunufaisha bayoanuwai, uoto, watu na – hatimaye tabianchi yetu.

23 Hans drone 12 2023 Bunds Selela Monduli _ Arusha Tanzania

Kuna jumla ya hifadhi 5 za mbegu za nyasi

Katika hifadhi zetu za mbegu za nyasi, wanawake wanapanda, wanavuna na wanauza nyasi (nyasi kavu) na mbegu. Wanajipatia kipato kwa kuziuza kwenye masoko yao au katika mashirika. Hifadhi za mbegu za nyasi hutengeneza kichaka cha kijani jangwani, na nyasi kavu wanayoyavuna akina mama hutumika kama chakula cha mifugo yao nyakati za ukame.

Uuzaji wa nyasi na mbegu za nyasi zilizovunwa kutoka kwenye hifadhi za mbegu za nyasi huwatengenezea kipato wanawake wanaotunza hifadhi hizo. Kipato hiki hutumika kama mbadala wa kuendesha maisha, na kuwafanya wanawake wasiwe tegemezi.

Jumla ya wanawake 130 wanajihusisha na hifadhi hizi za mbegu za nyasi.

Grass seed bank

Zaidi ya watu elfu 10 wananufaika

Kuwezesha watu, mmoja baada ya mwingine, katika kukijanisha ardhi yao ni mbinu yenye gharama nafuu, mbinu madhubuti na ni kichocheo cha mabadiliko ya kijamii na kiuchumi. Ili kutimiza jambo hili, tunahitaji kufahamika kwa watu. Hivyo, tunahamasisha wakulima kwa kuwaonesha faida za kuboresha ardhi sambamba na kuwapa mbinu za jinsi ya kuanza.

1809_Kisiki Hai 6people_tanzania_trees_marc_haers (1)

Mbinu yetu

Matuta ya kuvunia maji
Hifadhi za mbegu za nyasi
Fanya Juu na Fanya Chini
Usimamizi wa malisho
Kuhamasisha mbinu za matumizi endelevu ya ardhi

Matuta ya kuvunia maji

Matuta ya kuvunia maji ni makingamaji ya nusu duara yanayotengenezwa kwa ajili ya kufunua tabaka gumu la juu la udongo.

Matuta haya hupunguza kasi ya maji na hutumika kuvuna maji yanayotiririka kutoka milimani, na kuzuia mmomonyoko wa udongo wenye rutuba. Pia, hurejesha mlinganyo wa maji katika udongo, hali inayoongeza upatikanaji wa maji kwa ajili ya mbegu ambazo bado zipo ardhini. Mbegu hizi sasa zinapata nafasi ya kuota, yaani: ukijanishaji! Katika Mradi wa Mazingira wa eneo la katikati ya Tana, jamii ya Kimasai tayari imeshachimba zaidi ya matuta 50.000 ya kuvunia maji!

decorative image

Hifadhi za mbegu za nyasi

Hifadhi za mbegu za nyasi ni sehemu ndogo ya ardhi ya jamii ambayo hutumika katika uzalishaji wa nyasi na mbegu za nyasi.

Hifadhi za mbegu za nyasi zinasimamiwa na kuhudumiwa na vikundi vya wanawake wa Kimasai. Nyasi zikikomaa vizuri, nyasi hizo hutoa mbegu ambazo huuzwa na wanawake kwenye masoko yao au katika miradi mingine ya ukijanishaji. Hii husaidia kuongezeka kwa pato la wanawake pamoja na kijani kibichi katika maeneo mengine, jambo lenye faida kwa pande zote mbili!

decorative image

Fanya Juu na Fanya Chini

Fanya Juu na Fanya Chini ni mbinu zinazotumika kuvunia maji ya mvua. Wakulima huchimba makinga maji katika mashamba yao ili kuzuia mmomonyoko na kuvuna maji ya mvua ambayo ni muhimu katika ardhi zao.

Fanya Chini maana yake ni ‘tupa udongo upande wa chini’. Hii huzuia  maji ya mvua kutoka nje ya shamba kuingia shambani, jambo linalozuia mmomonyoko wa udongo wenye rutuba. Fanya Juu inamaanisha ‘tupa udongo upande wa juu’, huzuia maji ya mvua katika shamba yasitoke shambani, jambo linaloongeza upatikanaji wa maji kwa ajili ya mazao. Mwishowe, huwasaidia wakulima kukijanisha zaidi mashamba yao!

decorative image

Usimamizi wa malisho

Ili kuhakikisha miradi inakuwa endelevu, tutaanzisha mpango wa usimamizi wa malisho kwa kushirikiana na washirika wetu waliopo katika maeneo husika pamoja na jamii.

Lengo ni kuzuia ufugaji wa mifugo mingi kupita kiasi katika maeneo yaliyoharibiwa na yale yaliyo katika hatari ya kuharibiwa. 

Farmer with livestock

Kuhamasisha mbinu za matumizi endelevu ya ardhi

Ili kuongeza nguvu yetu katika uboreshaji wa mazingira, tunahamasisha utekelezaji wa mbinu mbalimbali za matumizi endelevu ya ardhi katika jamii, ikiwa ni pamoja na usimamizi wa machungio, udhibiti wa viumbe hatari pamoja na matumizi ya mbinu za kuzuia mmomonyoko.

Tunatekeleza haya kwa kutoa mafunzo, kuandaa mikutano ya vijiji, na kutumia njia mbalimbali za mawasiliano zinazojikita katika usambazaji wa maarifa na uhamasishaji. Kwa kuwahamasisha wanajamii kujaribu na kutumia mbinu za matumizi endelevu ya ardhi, tumeweza kulifanya eneo husika kuwa la kijani na lenye afya.

decorative image
poster

UNAWEZA SASA KUTEMBELEA MAENEO YETU YA MRADI!

Ili kuona kuona kutatua jinsi suluhisho zinazotegemea asili zinavyobadilisha, kanuni za ikolojia, na maisha ya jamii kwa ujumla, ni muhimu macho yako mwenyewe.

Lakini hapo ndipo changamoto inapoanza: hatuwezi kuleta watu wote duniani kwenye miradi yetu. maana tumeunda suluhisho hili la kupita kupitia uzoefu wa mwingiliano. Tumefanya maajabu ya miradi yetu ya kijani kibichi yaweze kufika moja kwa moja kwako—popote ulipo!

DHAMIRA YETU

Tuko kwenye dhamira ya kuhamasisha mamilioni ya watu kuchukua hatua kurekebisha hali ya kijani kibichi katika Afrika

Ikiwa tunataka kupooza sayari kwa muongo mmoja, kila mtu anahitaji kuwa kwenye mabadiliko. Kupitia nguvu ya vyombo vya habari, mawasiliano, taarifa, na teknolojia ya kisasa tunaweza kueneza ujumbe wetu na kuongeza kiwango. Tunataka kuhamasisha, kuunganisha na kuwezesha kizazi kizima, kukuza harakati za kurudisha mazingira.

KAZI NYINGINE

Kazi zetu zote