Miradi ya kukijanisha
Dodoma, Tanzania
MIAKA 10 IJAYO
Tuna dhamira ya kukijanisha Afrika ndani ya miaka kumi ijayo, pamoja na mamilioni ya wakulima na pamoja na wewe.
Fikiria kuweza kuwahamasisha na kuwawezesha mamiloni ya wakulima wadogo kurejesha ardhi zao kwa kutumia mbinu zilizo thibitika za usimamizi endelevu wa matumizi ya ardhi.
Je! Unaweza kufikiria athari kubwa ambayo itakuwa nayo katika upatikanaji wa mavuno ya mazao, mapato ya kaya, bioanuwai, upatikanaji wa maji, hali ya hewa ya maeneo husika na mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni? Na inaweza kufanyika, badala ya kusonga polepole kutoka eneo moja hadi lingine ardhini, kwa kuhamasisha kila mtu pamoja katika harakati moja iliyounganishwa, ya kimataifa?
Inayoleta pamoja mashirika yasiyo kiserikali , serikali, na makampuni ndiyo ambayo yameunganisha mkulima ndani ya Senegal na mwingine ndani ya Malawi?
Ndani ya Justdiggit, dhamira yetu ni kukijanisha Africa ndani ya muongo mmoja ujao, na lengo letu ni kuhamasisha na kuwapa watu nguvu ulimwenguni kote kujiunga nasi.
Kazi zetu zinajumuisha kufungamanisha mbinu za kuongoa mandhari ya ardhi na nguvu ya vyombo vya habari , mawasiliano, taarifa na tekonolojia ya simu. Juhudi zetu za kuongoa ardhi kwa kupitia mtandao mkubwa wa vyombo vya habari vya kimataifa kwa ajili ya kupanua wigo. Pia tunashirikiana na washirika wa ndani, kitaifa na kimataifa na wenye juhudi
Over twZaidi ya theluthi mbili ya ardhi barani Afrika imeharibika. Walakini, Afrika pia ina uwezo mkubwa zaidi wa kurejesha uoto katika mabara yote kwenye sayari yetu nzuri, na fursa ya kulinda na kurudisha bionuwai kwa baadhi ya mifumo ya ikolojia yenye thamani zaidi ulimwenguni. Ndio maana tunazingatia Afrika.
Katika program zetu zote za kurudisha mazingira tulizonazo, tunatafuta njia bora za kushirikiana kwa karibu na washirika na jamii. Faida dhahiri ya kijamii na kiuchumi kwao pia inatiwa moyo kwa kuhusishanisha vitu hivo ili tuweze kuhakikisha mipango hiyo ni endelevu.
Watu wakisherekea wakati tamasha la utengenezaji wa mvua Tanzania. 2019
Tazama hadithi yetu
Ikiwa tunataka kuipooza sayari kwa muongo mmoja, kila mtu anahitaji kuwa kwenye mabadiliko. Nguvu ya vyombo vya habari, mawasiliano, taarifa na teknolojia ya kisasa hutumiwa kueneza ujumbe wetu na kuongeza wigo.
Lengo letu ni kuhamasisha, kuunganisha na kuwezesha kizazi kizima, kukuza harakati za kurudisha mazingira.