MAJARIDA NA FILAMU
ANGALIA NA UJIFUNZE
ANGALIA FILAMU ZETU
NA MAJARIDA
Waongozaji wazuri wa filamu vijana wamekuwa wakifanya kazi nasi kufanikisha hii. Katika filamu na majarida yetu tunaonyesha njia yetu ya kurudisha asili, na matokeo ya kuvutia suluhisho rahisi la kukijanisha. Tazama sinema zetu hapa:
TUNATENGENEZA SANAA YA FILAMU NA MAJARIDA KUHUSU MIRADI YA KUKIJANISHA.
Hadithi za wakulima: utangulizi
Ndani ya mfululizo huu watu kadhaa waliohusika katika mradi wa kurejesha kijani kibichi huko Monduli, Tanzania wanashiriki uzoefu wao binafsi katika mfululizo wa mahojiano.
Hadithi za wakulima: sehemu ya 2
Katika kipindi hiki cha pili tunapata kujua utoto, matumaini na matakwa ya watu wanne waliohusika katika mradi huo.
UTENGENEZAJI WA MVUA I: JARIDA LA JUSTDIGGIT
Jarida hili fupi la Justdigit linaonyesha miradi inayoendelea, kuchimba makinga maji ya nusu mwezi 72.000 kwa ajili ya kuvuna maji ya mvua na kurejesha ardhi iliyo haribika.
UTENGENEZAJI WA MVUA II: MBEGU ZA MABADILIKO
Mfuatano wa tuzo za ushindi za jarida la utengenezaji wa mvua. Ambapo utengenezaji wa mvua una onyesha kuanza kwa miradi ya Just dig it na umuhimu wake, mbegu ya mabadiliko inaonyesha hatua tulizopiga na jinsi gani kukijanisha kuna faidisha sisi sote.
UTENGENEZAJI WA MVUA III: HADITHI YA TANZANIA
Utengenezaji wa mvua III unaeleza hadithi kuhusu kusambaza mawazo ambayo yanaweza kurudisha mamilioni ya miti kurudi hali ya uhai. Kisiki Hai! Ujumbe wa matumaini na chanya. Inaonyesha faida chanya za miti katika namna tofauti. Unataka kujua kuhusu hizi faida? Angalia jarida letu!
Kisiki Hai I
Hamasika!
Ndani ya sinema hii ya elimu unajifunza yote juu ya athari chanya za Kisiki Hai. Yona, mkulima anayeishi mkoa wa Dodoma, anamtembelea mkulima Augustino, ambaye anatekeleza njia ya Kisiki Hai kwenye shamba lake kwa miaka mingi. Yona anagundua kuwa kurudisha miti kwenye ardhi yako kunaweza kuifanya ardhi yako kuwa ya kijani na yenye rutuba tena, na kuifanya iwe rahisi sana kukuza mazao. Unataka kujua jinsi ardhi iliyojaa miti inaweza kuonekana? Tazama sinema ya Kisiki Hai I!
Kisiki Hai II
Hamasika!
Ndani ya Kisiki Hai II unajifunza hatua nne tofauti za Kisiki Hai, inayokuwezesha kuitumia kwenye ardhi yako mwenyewe. Unajifunza msaada wa kumbukumbu, ukihakikisha unaweza kukumbuka hatua zote kwa urahisi. Mbinu mpya ya kukijanisha miti huletwa pia, Fanya Juu na Fanya Chini, ikikusaidia kuvuna maji ya mvua yanayoanguka kwenye ardhi yako. Hii inaongeza upatikanaji wa maji kwa mazao, kuhakikisha inaweza kukua vizuri. Tazama sinema hii ya elimu na uanze mwenyewe!