Kujenga ushirikiano wa vyombo vya habari
Kukuza ufahamu wa njia za asili kwenye kiwango cha kimataifa, tunaunda kampeni chanya za uelimishaji mtandaoni na nje ya mtandao. Ndani ya ulaya lengo la kampeni hizi Zaidi ni kujenga uelewa kati ya umma kwa jumla. Barani Afrika, lengo letu ni kuhamasisha mamilioni ya wakulima kuanza kukijanisha ardhi zao.
Havas Media na JCDecaux, mashirika yote mawili yanayoongoza katika tasnia ya habari na mawasiliano, yameunga mkono Justdiggit kwa miaka ndani ya Ulaya. Ushirikiano huu umeongezwa kwa miradi yetu ya Afrika kwa vyombo vya habari kujitolea na msaada wa kimkakati katika uwezekano wa kila nchi ya Kiafrika ambapo wanafanya kazi.
Msaada huu unamaanisha tunaweza kukuza mtandao wa media katika nchi mbalimbali, ikijumuisha kila aina ya washirika wa kitaifa na wa ndani. Matokeo? ? Nafasi ya matangazo iliyofadhiliwa katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni pamoja na luninga, redio, mabango, sinema, na msaada wa hiari wa mabalozi wetu wakuu, washawishi, na wengine wengi.