UNAHITAJI ARDHI ILIYOBOREKA KWA AJILI YA KUPANDA MAZAO BORA?

Anza kukijanisha ardhi yako leo!

Kukijanisha na kurejesha ardhi iliyoharibiwa ni rahisi na  njia yenye ufanisi! Kwa kutumia mbinu rahisi, unaweza kukuza mimea haraka na kutengeneza udongo wenye rutuba kwa mazao yako, au nyasi endelevu kwa ajili ya mifugo yako. Unahisi kuhamasika? Chimba na anza kuirudisha ardhi yako leo, pamoja na maelfu ya wakulima wengine na wafugaji.

Je unahitaji kufahamu na kwanini ardhi yako inakuwa kavu na isiyo na rutuba, na jinsi gani njia za kurejesha uoto kama Kisiki Hai pamoja na kuchimba makinga maji itasaidia? Angalia filamu zetu.

rainmakers trailer still

Je unafahamu kukijanisha ni rahisi? Ni suala la kuchagua mbinu sahihi kwa ardhi sahihi. Jifunze mbinu tofauti tofauti tunazotumia kuifanya ardhi kavu kuwa ya kijani tena.

What we do Treecovery

Pamoja na Farm Radio International Pamoja na Dodoma FM tumetengeneza kipindi mahsusi cha redio. Katika kipindi hicho utajifunza zaidi kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi, athari chanya za Kisiki Hai na jinsi gani unaweza kufanya peke yako.

Farm radio show - Kisiki Hai Tree

Kabla ya kuanza kukijanisha, ni muhimu kufahamu mazingira yako, ardhi Pamoja na hali ya hewa. Pindi utakapojua aina ya mandhari ya ardhi yako, jifunze kuhusu mbinu  ambayo itakufaa katika kukijanisha ardhi.

Man digging water bund

Kutuma mafanikio yako kupitia mitandao ya kijamii pia inaweza kusaidia kuhamasisha wakulima wengine na wafugaji. Onyesha picha ya ardhi yako mpya iliyokijanishwa  na uwaambie watu juu ya faida za kukijanisha. Angalia ukurasa wetu wa Instagram au Facebook kwa  kuhamasika! Unahitaji msaada? Acha tuwasiliane.

Movie Roadshow Tanzania people village

Je unahitaji kukijanisha ardhi yako? Tunaweza kukupa mkono. Aina yetu ya vifaa ( maelekezo yetu  ya luninga, michoro ya jinsi ya kukijanisha na zaidi) inaweza kukusaidia kuanza.

Shovel in green bund

WASILIANA NASI KWA SWALI LOLOTE AMBALO UNAWEZA KUWA NALO.