Ni wakati wa kusambaza neno na kusambaza ukijani

Tunataka kuufahamisha ulimwengu kuwa njia za asili ni ufunguo katika kugeuza mabadiliko ya hali ya hewa, na kuhamasisha kila mtu kushiriki katika kufanya mabadiliko hayo kutokea.

Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, tumethibitisha kuwa inawezekana kurudisha mandhari iliyoharibika katika  ukanda wa jangwa la sahara Afrika kwa haraka na kwa ufanisi. Kwa kuhamasisha wakulima zaidi na athari chanya juu ya ardhi na watu, sasa tunahamia hatua inayofuata:. Kukijanisha kwa Ubunifu.

KaiOS Justdiggit

Wakulima wameshariki katika programu ya majaribio ya kijanisha, Tanzania

  • 1. Program za kukijanisha
  • 2. Kuongeza uwezo
  • 3. Kampeni za kidunia kuhusu uelewa

Programu za Kukijanisha

Tunaendesha programu za kukijanisha kwenye ardhi barani Afrika, ambapo tunatumia mbinu za asili zinazoweza kukua na rahisi kutumia katika kurudisha mazingira. Ili kueneza zaidi mbinu hizi na kuzikuza  programu zetu, zinatumia vyombo vya habari, taarifa, teknolojia na mawasiliano.

Pamoja na jamii na washirika wa ndani, maeneo yaliyotengwa yamekijanishwa kwa njia ya haraka na endelevu. Hii inaboresha maisha, na ina athari chanya kwenye bioanuwai na mabadiliko ya hali ya hewa. Wakati huo huo, programu hizi ndio ambapo maoni na ubunifu mpya hujaribiwa na kutathminiwa.

temperature soil vierkant

Kuongeza nguvu ya mawasiliano na teknolojia

Tunajua njia ya kukijanisha inafanya kazi na tunajua jinsi inavyofanya kazi.

Hatua inayofuata ni kusambaza maarifa haya, kwa kutumia teknolojia (ya rununu) kuhamasisha, kuelimisha na kuwawezesha wakulima kurejesha ardhi yao wenyewe kwa kutumia mbinu rahisi, bila hitaji la uwepo wetu sehemu husika. Shukrani kwa ukuaji mkubwa na kupenya kwa mtandao na teknolojia ya rununu barani Afrika, sasa tunaweza kuwawezesha wakulima mahali popote Kusini mwa Jangwa la Sahara kukijanisha ardhi zao.

Taking a picture of the bund

Kampeni ya uelewa kidunia

Ikiwa tunataka kupooza sayari katika muongo mmoja, kila mtu anahitajika kuwa kwenye mabadiliko na tunahitaji kuonekana kila mahali: Katika habari, matangazo, vituo vya kijamii, mazungumzo, na zaidi ya yote katika mioyo na akili za watu.

Tunatumia nguvu ya vyombo vya habari na mawasiliano kuunda uelewa na ufahamu na kutoa suluhisho halisi wakati wa mabadiliko ya hali ya hewa. Kampeni zetu za kimataifa za uelimishaji kwenye mtandao na nje ya mtandao zinatengenezwa ili kukuza njia za asili na kuhamasisha, kuunganisha na kuwezesha kizazi chote, kukua katika harakati za kuongoa mazingira.

decorative image