Jifunze hatua za
Fanya Juu na Fanya Chini

Jifunze hatua za Fanya Juu na Fanya Chini, ili uweze kutumia njia hii katika shamba lako. Kwa kupitia hii njia unachimba makinga maji katika shamba lako ili uweze kuvuna maji ya mvua.

Tekeleza mwenyewe!

poster

Nini Maana ya
Fanya Juu na
Fanya Chini?

Kwa kutumia njia ya Fanya Juu na Fanya Chini, una chimba makingamaji katika shamba lako ili kuvuna maji ya mvua.

Fanya Chini ni Kingamaji ambalo linachimbwa upande wa juu wa shamba, udongo uliochimbwa unawekwa upande wa chini ili kutengeneza tuta ambalo litazuia maji kutoka mlimani kuingia shambani ili kuzuia mmomonyoko wa udongo wenye rutuba.

Fanya Juu ni kingamaji ambalo linachimbwa upande wa chini wa shamba, udongo uliochimbwa unawekwa upande wa juu wa shamba ili kutengeneza tuta ambalo litasaidia kubakiza maji ya mvua shambani na kuongeza upatikanaji wa maji kwa mimea. Mwishoni inasaidia kukijanisha ardhi yako!

Jifunze hatua za Fanya Juu na Fanya Chini, ili uweze kutumia njia hii katika shamba lako:

 • HATUA 1: Angalia
 • HATUA 2: Pima
 • HATUA 3: Tafuta nguvu kazi
 • HATUA 4: Chimba
 • HATUA 5: Imarisha
 • HATUA 6: Tunza

HATUA 1: Angalia

Baini uelekeo wa mtiririko wa maji katika shamba lako kwa kuangalia au kwa kutumia vipimo.

 • Fikiria sehemu ambayo ungependa kuweka Fanya Juu au Fanya Chini ili kuzuia mtiririko wa maji.
 • Kwa kawaida, huwa kuna umbali wa mita 10 mpaka 20 kati ya kingamaji moja la Fanya Juu au Fanya Chini na kinga maji lingine kulingana na kasi ya mteremko. Idadi na mpangilio wa makinga maji hupatikana wakati wa upimaji.
 • Hakikisha angalau una kingamaji moja upande wa juu la shamba lako na lingine upande wa chini ya shamba lako, lakini idadi hii yaweza ongeza kulingana na kasi ya mteremko.
decorative image

HATUA 2: Pima

Pima na chora mistari kwenye ardhi.

Tumia vifaa vya kupimia na uchore mistari kwenye ardhi sehemu ambayo utachimba Fanya Juu au Fanya chini ili kuzuia mtiririko wa maji.

decorative image

HATUA 3: Tafuta nguvu kazi

Tafuta watu wakusaidie kuchimba.

Kwa mfano unaweza kutengeneza kikundi cha watu wanaoweza kushirikiana kuchimba makingamaji: kikundi kifanye kazi katika shamba la mwanakikundi mmoja hadi pale kila mwanakikundi atakapokuwa na makingamaji katika eneo lake au unaweza kuajiri watu wakufanyie kazi/kutumia mashine ya kuchimba: ni njia ya uwekezaji kwa sababu makinga maji yataongeza mavuno na kukupa kipato zaidi.

decorative image

HATUA 4: Chimba

Chimba makingamaji.

 • Kila kingamaji linatakiwa kuwa na upana wa sentimita 60 na kina cha sentimita 60.
 • Chimba kingamaji na kila baada ya mita kumi acha banio lenye urefu wa mita moja.
 • Katika eneo la upande wa juu wa shamba lako chimba Fanya Chini; weka udongo uliochimbwa upande wa chini ili kutengeneza tuta ambalo litasaidia kuzuia maji kutoka mlimani.
 • Katika eneo la chini wa shamba lako chimba Fanya Juu; weka udongo uliochimbwa upande wa juu ili kutengeneza tuta ambalo litasaidia kubakiza maji na udongo ndani ya eneo lako; hii italeta mazingira mazuri kwa mazao yake.
decorative image

HATUA 5: Imarisha

Imarisha matuta.

Panda nyasi au mimea mingine yenye mizizi yenye nguvu kwenye tuta.

decorative image

HATUA 6: Tunza

Tunza makingamaji.

Hakikisha unakagua makinga maji katika kipindi cha kuandaa shamba na kipindi cha mavuno. Kila mwaka toa udongo ulioingia ndani ya kingamaji.

decorative image