Kutana na
wachimbaji

Tunachimba makinga maji katika msimu wa kiangazi.

Katika kipindi hiki, kikundi cha wanajamii hufanya kazi kwa bidii katika kukomboa ardhi yao kavu na iliyoharibika kwa kuchimba makinga maji. Kwa ujumla, wanachimba maelfu ya makinga maji katika eneo hilo ili kufanya eneo kuwa la na baridi tena. Hebu tukuarifu  kidogo zaidi juu yao na jinsi siku hasa ya kuchimba makinga maji  inaonekanaje.

Siku ya kuchimba

Diggers walking to the project area

1. Kuwasili kwenye eneo la mradi

Kila siku ya kuchimba, asubuhi na mapema wanajamii hutembea hadi eneo la mradi. Wote wanaishi karibu, ili waweze kufika eneo hilo kwa urahisi kwa miguu. Je, ungependa kujua safari hii inaonekanaje? Ione hapa.

Wakishafika katika eneo hilo, wanajamii wataanza kuchimba makinga maji.

digging bunds

2. Kuchimba makinga maji

Kabla ya uchimbaji kuanza, fundi (msimamizi ndani ya mradi) huchora mtaro wa kila kinga maji chini kwa kutumia pima maji. Kwa njia hii makinga maji  huchimbwa sehemu sahihi na yatavuna maji mengi iwezekanavyo. Na kisha kazi halisi huanza: kuchimba makinga maji!

Kila siku, kila mwanachama huchimba makinga maji 7 ya nusu duara yenye upana wa mita 5, urefu wa mita 2.5 na kina cha mita 0.5. Hebu fikiria ni mita ngapi kila siku! Unashangaa jinsi mchakato wa kuchimba  makinga maji unaonekana? Tazama mpangilio wa muda.

women seeds

3. Kukuza asili

Wakati mwingine, asili inahitaji mkono wa kusaidia kukua na ukijani tena. Ndiyo maana wachimbaji mara kwa mara hupanda mbegu za nyasi ndani ya makinga maji mapya yaliyochimbwa. Mara tu makinga maji yanapovuna maji ya mvua, mbegu huanza kuota na kukijanisha huanzaia hapo. Nyasi hizi mpya  zinavumilia, na kuhakikisha kuwa eneo hilo linabaki kuwa la kijani.

Ukweli wa kufurahisha: tunanunua mbegu hizi za nyasi kutoka kwa vikundi vya wanawake wa Kimasai vinavyoendesha miradi yetu ya hifadhi ya mbegu za nyasi nchini Kenya.

Kenya bund digging mobile

4. Tabasamu la dunia

Baada ya makinga maji  kuchimbwa na mbegu za nyasi kupandwa, zikiwa tayari kunaswa na kamera: wasimamizi huchukua picha ya kila kinga maji moja katika eneo la mradi na kuzirusha kwenye Programu ya Dig. Kila moja ya picha ya haya makinga maji itakabidhiwa kwa mwekezaji (wewe). Kwa njia hii, unapoingia kwenye Jukwaa letu la kukijanisha, unaweza kuona picha yako ya kinga maji la kipekee! Na kisha… Mchakato wa kuongeza kukijanisha huanza. Mvua ya kwanza inaponyesha, mimea huanza kuchipua ndani ya makinga maji. Hatimaye, makinga maji yote kwa pamoja hugeuza eneo kavu na lililoharibiwa kuwa kijani na baridi tena.

Watu wengine wanaohusika

Kenya_Enkii_Tony Wild_digging_portrait_action_bunds_people_shovel_Maasai_APK_OCTOBER_20-88

Fundi

Fundi ni msimamizi wa miradi ya makinga maji.. Wanahakikisha kuwa makinga maji yamechimbwa kwa usahihi na kuchukua picha za kinga maji lilichochimbwa. Picha hizi hurushwa kwenye Jukwaa la kukijanisha ambapo zimeunganishwa na mnunuzi wa kinga maji.

Lenayia in Inkisanjani project area

Wasimamizi wa mradi

Ili kuendesha miradi ya  makinga maji vizuri, tuna wasimamizi wa mradi katika sehemu husika. Wasimamizi hawa wa mradi ndio sehemu kuu ya mawasiliano ya wachimbaji na wafadhili. Lenayia kutoka shirika letu washirika la MWCT ni mmoja wa wasimamizi wetu wa miradi katika miradi ya makinga maji.

Ranger with shovel

Walinzi

Kando na wachimbaji, pia tunafanya kazi na walinzi katika maeneo ya mradi. Wanalinda maeneo kutokana na malisho ya mifugo, kuhakikisha maeneo yanabaki kijani. Kando na hayo, pia wanalinda wanyamapori katika maeneo hayo dhidi ya majangili.

decorative image

NUNUA KINGA MAJI LAKO MWENYEWE!

Wekeza kwenye kipande chako cha kijani : Nunua makinga mengi upendavyo kupitia jukwaa letu la kukijanisha. Mara tu makinga maji yako yanapochimbwa, utapokea picha ya kipekee ya kinga maji lako mwenyewe.