Kurejesha miti kwa njia ya Karkaral

Kwa kushirikiana na washirika wetu katika ngazi ya chini kabisa, tunasaidia kueneza Kampeni ya Kisiki Hai nchini Senegali kwa kuhamasisha matumizi ya Karkaral: jina la asili la mbinu ya Kisiki Hai (FMNR) ambayo wakulima huitumia kurejesha miti, kuboresha ardhi zao na kuongeza uwezo wa kustahimili mabadiliko ya tabianchi.

Lengo la mradi wetu wa majaribio nchini Senegali ni kutathmini uwezo wa washirika, wakulima na jamii katika utekelezaji wa mradi wa Kisiki Hai, na kuangalia uwezekano wa kuongeza eneo la mradi.

Tumewapata washirika wenyeji eneo la katikati ya nchi, linalojulikana kama Peanut Bassin, lenye sifa ya historia ndefu ya utamaduni wa kilimo cha ulezi na mtama kama mazao makuu ya nafaka. Union Regionale des Associations Paysannes de Diourbel (URAPD), JIG JAM, na Regroupement Communautaire pour l’Auto Développement des Familles (RECODEF) kila moja lina nafasi yake muhimu katika ukijanishaji wa eneo hili. 

Kupitia programu yetu, tunafanya kazi katika mashamba mbalimbali katika jamii saba zinazopatikana eneo la katikati Magharibi mwa Senegali (Thies, Diourbel na Fatick). Msingi wa mbinu yetu katika kuboresha maisha, afya ya udongo na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika maeneo haya ni utoaji wa mafunzo kwa wakulima wanaojulikana kama machampioni. Machampioni ni wakulima wenye uzoefu na wanaoheshimika sana ambao huwa tunawapa mafunzo ya mbinu za Urejeshaji Asilia Unaosimamiwa na Mkulima (FMNR) (mfano, Kisiki Hai), na kuwajengea uwezo wa kuwafundisha mbinu hizi wakulima wote katika vijiji vyao.

Faida zinazotarajiwa kupatikana Eneo la Katikati Magharibi mwa Senegali

24.000 Hekta

za ardhi zinazoboreshwa

960.000

Miti iliyorejeshwa

6.000

Wanakaya waliopewa mafunzo

Katika programu yetu tunakusudia kuboresha hekta 24.000

Kwa kutumia mbinu za kizamani na za kisasa zinazoangazia usimamizi wa malisho na uvunaji wa maji ya mvua, tunataka kuboresha hekta 24.000 za ardhi iliyoharibiwa katika eneo la katikati Magharibi mwa Senegali.

Urejeshaji wa uoto una faida nyingi katika tabianchi, katika mazingira na bayoanuwai, kwa binadamu na maisha yao.

7(option 2)_more regreening techniques_landscape restoration_what we do_Justdiggit_dig in_shovel_green_vegetation

Tunatarajia kurejesha miti laki 960.000 kwa kutumia mbinu ya Kisiki Hai

Tunarejesha visiki vya miti vilivyosahaulika kwa kutumia mbinu inayoitwa Urejeshaji Asilia Unaosimamiwa na Mkulima (FMNR), au kama tunavyopenda kuiita: Karkaral nchini Senegali. Mbinu hii ina ufanisi zaidi kuliko kupanda miti mipya! Lengo ni kurejesha jumla ya miti 960.000 katika Eneo la katikati Magharibi mwa Senegali.

Kwa kuirejesha miti hiyo, tunaweza kuboresha maeneo yaliyoharibiwa na kuyafanya maeneo hayo kuwa ya kijani na matulivu kama mwanzo.

Kisiki Hai Treecovery _ Manyara Tanzania

Tunatarajia watu 6.000 watanufaika na programu yetu

Washirika wote watatu watafanya kazi katika vijiji 10, na kutakuwa na mkulima championi mmoja kwa kila kijiji, atakayewafundisha na kuwasaidia wakulima 200. Hii itafanya kuwe na jumla ya wakulima 6.000 watakaofikiwa na programu wakati wa majaribio.

1809_Kisiki Hai 6people_tanzania_trees_marc_haers (1)

Mbinu yetu

Karkaral
Kuwajengea uwezo
Kuhamasisha mbinu za matumizi endelevu ya ardhi

Karkaral

Urejeshaji Asilia Unaosimamiwa na Mkulima (FMNR), au Karkaral nchini Senegali, ni mbinu ya kukuza tena miti na kutunza miti mipya, machipukizi ya miti yanayochipua na kuwa miti mikubwa.

Pamoja na mpango huo wafugaji wa ndani na wakulima wanafunzwa kutumia mbinu hiyo kwenye ardhi yao wenyewe, kuruhusu kuota upya kwa miti 480.000 inayotarajiwa.

kisiki hai regreening tanzania

Kuwajengea uwezo

Kwa kuwapa mafunzo wawezeshaji 30 (wanaoitwa machampioni wa ‘kukijanisha’), tunaweza kuwafikia wakulima katika vijiji 3.000 katika mkoa wa Katikati Magharibi mwa Senegali.

Wawezeshaji hawa huwafundisha wakulima wenzao jinsi ya kurejesha miti katika mashamba yao. Kwa kufanya hivi, maelfu ya wakulima wamehamasishwa kukijanisha ardhi zao, na kurejesha mamilioni ya miti katika mkoa wa Katikati Magharibi mwa Senegali na kuongezeka uwezo kukabiliana na ukame, uzalishaji wa chakula na pato la kaya. Machampioni wa kukijanisha pia wamefundishwa mbinu za uvunaji wa maji ya mvua, na kuwawezesha kukijanisha zaidi ardhi zao.

decorative image

Kuhamasisha mbinu za matumizi endelevu ya ardhi

Ili kuongeza nguvu yetu katika uboreshaji wa mazingira, tunahamasisha utekelezaji wa mbinu mbalimbali za matumizi endelevu ya ardhi katika jamii, ikiwa ni pamoja na usimamizi wa machungio, udhibiti wa viumbe hatari pamoja na matumizi ya mbinu za kuzuia mmomonyoko.

Tunatekeleza haya kwa kutoa mafunzo, kuandaa mikutano ya vijiji, na kutumia njia mbalimbali za mawasiliano zinazojikita katika usambazaji wa maarifa na uhamasishaji. Kwa kuwahamasisha wanajamii kujaribu na kutumia mbinu za matumizi endelevu ya ardhi, tumeweza kulifanya eneo husika kuwa la kijani na lenye afya.

Meeting grass seed bank
poster

UNAWEZA SASA KUTEMBELEA MAENEO YETU YA MRADI!

Ili kuona kuona kutatua jinsi suluhisho zinazotegemea asili zinavyobadilisha, kanuni za ikolojia, na maisha ya jamii kwa ujumla, ni muhimu macho yako mwenyewe.

Lakini hapo ndipo changamoto inapoanza: hatuwezi kuleta watu wote duniani kwenye miradi yetu. maana tumeunda suluhisho hili la kupita kupitia uzoefu wa mwingiliano. Tumefanya maajabu ya miradi yetu ya kijani kibichi yaweze kufika moja kwa moja kwako—popote ulipo!

Ingia sasa na ujionee uzuri wa shamba la Treecovery kwa macho yako mwenyewe.

DHAMIRA YETU

Tuko kwenye dhamira ya kuhamasisha mamilioni ya watu kuchukua hatua kurekebisha hali ya kijani kibichi katika Afrika

Ikiwa tunataka kupooza sayari kwa muongo mmoja, kila mtu anahitaji kuwa kwenye mabadiliko. Kupitia nguvu ya vyombo vya habari, mawasiliano, taarifa, na teknolojia ya kisasa tunaweza kueneza ujumbe wetu na kuongeza kiwango. Tunataka kuhamasisha, kuunganisha na kuwezesha kizazi kizima, kukuza harakati za kurudisha mazingira.

KAZI NYINGINE

Kazi zetu zote