KUCHIMBA ILI
KUKIJANISHA

Kwa kuchimba makinga maji zaidi ya 360, 000, tumeweza kurudisha uoto katika ranchi ya kikundi cha Kuku, imetengeza faida za kimazingira na kutengeza ardhi kuwa yenye matumizi tena kwa jamii.

Ranchi ya Kuku Group iko kusini mwa Kenya na inafanya kazi kama ukanda muhimu wa wanyamapori kati ya Hifadhi ya Kitaifa ya Amboseli na Hifadhi ya taifa ya Tsavo. Ranchi ya kikundi ni nyumbani kwa watu wa Kimasai karibu 29,000 ambao wanategemea zaidi ardhi kama chanzo kikuu cha mapato na chakula. Kwa sababu ya malisho kupita kiasi na hali ya hewa inayobadilika, eneo hilo limekuwa kavu sana, na hivyo kuwa ngumu kwa jamii za eneo hilo kuishi kutokana na ardhi.
Pamoja na jamii ya Wamasai na mshirika wetu, Maasai Wilderness Conservation Trust (MWCT), tulianza kurejesha ardhi hii iliyoharibika. Kwa kuchimba makinga maji ya kuvuna maji ya mvua na kuanzisha benki za mbegu za nyasi, tunakijanisha hekta 3834 katika eneo hilo. Mpaka sasa jamii ya Wamasai imechimba makinga maji 369,000 ya maji na kuanzisha benki 7 za mbegu za nyasi, ambazo zinasimamiwa na vikundi vitano vya wanawake.

ATHARI NDANI YA KUKU
MPAKA SASA

29,000 +

Watu 29,000 wananufaika

Hekta 3834

tayari zimerejeshwa

7

Benki 7 za mbegu za nyasi

360,000 +

Makinga maji 360,000 yamechimbwa

126

Wanawake 126 wanahusika katika benki ya mbegu za nyasi

ZAIDI YA WATU 29,000 WANANUFAIKA NA MIRADI YETU

Zaidi ya watu 29 elfu wanaishi ndani ya ranchi ya Kuku. Wote wananufaika moja kwa moja na mbinu zetu za kurejesha uoto kutoka kwenye miradi yetu.

Kisiki Hai 2 - Tanzanian version.mp4.00_17_31_02.Still001

NDANI YA MIRADI YETU TUMEREJESHA HEKTA 3834

Kwa msaada wa mbinu za zamani na mpya zinazozingatia usimamizi wa malisho na uvunaji wa maji ya mvua, tunarejesha hekta 3834 za ardhi iliyoharibika ndani ya Kuku.

Kurejesha uoto  kuna athari nyingi chanya kwa hali ya hewa, mazingira na bioanuwai, kwa watu na maisha yao.

Kenia_Kuku_Before-After (2)

JUMLA YA BENKI TANO ZA NYASI NDANI YA KUKU

Ndani ya benki zetu za mbegu za nyasi, wanawake wa Kimasai hukua, huvuna, na kuuza nyasi  na mbegu. Wanapata mapato kwa kuuza kwenye masoko ya ndani au kwa mashirika. Hifadhi za mbegu za nyasi huunda eneo la kijani kibichi katika mazingira yaliyopoteza uwezo kuotesha tena uoto, na nyasi ambazo wanawake huvuna ni chakula cha mifugo yao wakati wa kiangazi.

Kwa jumla tuna benki 7 za mbegu za nyasi huko Kuku.

5_Kuku_ Kenya_Work_What we do_Justdiggit_kenya_Kuku_grass_seed_bank_women_Kilimanjaro

TUMECHIMBA MAKINGA MAJI ZAIDI YA LAKI MOJA 360 ELFU

Makinga maji (au kama tunavyopenda kuyaita: “tabasamu la dunia”) ni mashimo yenye umbo la nusu duara lenye kuvuna maji ya mvua.

Yanachimbwa katika maeneo yetu ya mradi barani Afrika ili kuvuna maji ya mvua ambayo vinginevyo yatapita juu ya ardhi kavu, isiyo ota kitu. Kwa kuchimba makinga maji, tunaweza kubadilisha eneo kubwa kwa muda mfupi sana, kufaidika kwa bioanuwai, asili, watu na – mwishowe hali ya hewa yetu.

6 juli 2020 bunds kenya drone (2)

KWA UJUMLA WANAWAKE 126 WANAHUSIKA KATIKA BENKI YA MBEGU ZA NYASI

Kuuza nyasi na mbegu za nyasi zilizovunwa kutoka kwenye benki za mbegu za nyasi hutengeneza chanzo cha mapato kwa wanawake ambao wanasimamia benki za mbegu za nyasi. Mapato haya hutumika kama njia mbadala ya kujipatia riziki, na kuwafanya wanawake wawe huru zaidi.

Kwa jumla wanawake 126 wanahusika katika Benki za Mbegu za Nyasi.

9(option 2)_landscape restoration_what we do_Justdiggit_womengroup_grass seed bank_OOGR_Kenya

NJIA ZETU

Makinga Maji
Mistari ya mawe
Hifadhi ya mbegu za nyasi
Kusimamia eneo la malisho

Makinga Maji

Makinga maji ni mashimo ya nusu duara kwa ajili kuifunua sehemu ya tabaka la juu la udongo.

Makinga maji yana punguza kasi ya maji na hatimaye kuvuna maji yanayo tiririka kutoka milimani. Ikizuia mmomonyoko wa udongo wa ardhi yenye rutuba. Mlinganyo wa maji kwenye udongo unakuwa sawa, inaongeza upatikanaji wa mbegu ambazo bado zipo kwenye udongo. Mbegu hizo sasa zinapata nafasi ya kumea juu ya ardhi nah io inamaanisha kukijanisha!

Green bund Kenya

Mistari ya mawe

Mistari ya mawe pia hutumiwa kuvuna maji ya mvua na kuzuia mmomonyoko wa udongo.

Inatumika katika maeneo ya Ranchi ya Kikundi cha Kuku ambapo mawe mengi yanapatikana. Mawe huvunja nguvu ya maji na huongeza upenyaji wa maji kwenye udongo. Nyenzo za kikaboni na mbegu hukamatwa nyuma ya mawe, ikitoa nafasi kwa mbegu kuweza kuchipua, na kukijanisha eneo.

Stone lines

Hifadhi ya mbegu za nyasi

Hifadhi za mbegu za nyasi ni sehemu ndogo ya ardhi ya jamii ambayo hutumiwa kwa uzalishaji wa nyasi na mbegu za nyasi.

Hifadhi ya mbegu za nyasi zinasimamiwa na kudumishwa na vikundi vya wanawake wa Kimasai. Nyasi zinapokua kabisa, nyasi hizo hutoa mbegu za nyasi ambazo zinauzwa na wanawake kwenye masoko ya ndani au kwa miradi mingine ya kukijanisha. Hii inamaanisha mapato zaidi kwa wanawake na kijani kibichi zaidi katika maeneo mengine, hali ya ushindi kwa pande zote!

Grass seed bank

Kusimamia eneo la malisho

Ili kuhakikisha uendelevu wa miradi , tulianzisha mpango wa usimamizi wa malisho pamoja na washirika wetu pamoja na jamii.

Lengo ni kuzuia kuchunga kupita kiasi katika maeneo yaliyorejeshwa hivi karibuni. Kupitia mpango wa uhamasishaji wa jamii, ushiriki  na uelewa wa jamii za wenyeji huhakikishiwa malisho. Tuliajiri pia walinzi wa jamii kulinda maeneo yaliyorejeshwa na maeneo yaliyo karibu.

Matokeo ya mradi huo ni ya kutia moyo, maombi ya kuongezewa miradi yanafanywa na jamii zote mbili pamoja na taasisi zisizo za kiserikali katika eneo hilo.

Farmer with livestock

Dhamira yetu

Tuko kwenye mpango wa kukijanisha Afrika kwa miaka 10 ijayo, Pamoja na mamilioni ya wakulima, na Pamoja na wewe.

Ikiwa tunataka kupooza sayari kwa muongo mmoja, kila mtu anahitaji kuwa kwenye mabadiliko. Tunatumia nguvu ya vyombo vya habari, mawasiliano, taarifa, na teknolojia ya kisasa kueneza ujumbe wetu na kuongeza kiwango. Tunataka kuhamasisha, kuunganisha na kuwezesha kizazi kizima, kukuza harakati za kurudisha mazingira.

Makala ya utengenezaji wa
mvua II

Mbegu ya mabadiliko

Tulitengeneza filamu mbili nchini Kenya kuonyesha athari za miradi yetu. Wakati sehemu ya kwanza ya safu ya Makala yetu ya utengenezaji wa mvua inaonyesha mwanzo wa miradi yetu na hitaji lao, Mbegu za Mabadiliko zinaonyesha matokeo ya wazi ya kukijanisha,  miradi yetu na athari chanya miradi yetu inayo kwa wanadamu na wanyama.

poster

KAZI NYINGINE

Kazi zetu zote