Benki ya Mbegu za Nyasi KUONGOA MANDHARI YA ARDHI

NINI MAANA YA HIFADHI YA MBEGU ZA NYASI?

Kuwawezesha wanawake na kurudisha tena uoto

Hifadhi za mbegu za nyasi ni sehemu ndogo ya ardhi ya jamii ambazo hutumiwa kwa uzalishaji wa nyasi na mbegu za nyasi. Nyasi ambazo zinakua kwenye hifadhi ya mbegu za nyasi zinalindwa kutokana na malisho ya mifugo na wanyama wa porini na kile kinachoitwa uzio unaoishi wa vichaka vya asili. Wanaunda eneo la kijani kibichi katika mazingira tasa!

Hifadhi ya mbegu za nyasi zinasimamiwa na kudumishwa na vikundi vya wanawake wa Kimasai nchini Kenya. Nyasi zinapokua kabisa, nyasi huzaa mbegu za nyasi ambazo zinauzwa na wanawake kwenye masoko ya ndani au kwa miradi mingine ya kukijanisha.

Grass seeds

HIFADI YA MBEGU ZA NYASI KAMA UJASIRIAMALI

Katika miradi yetu huko Kuku, Kenya & OOGR, Kenya tulianza kubadilisha hifadhi ya  mbegu za nyasi kuwa biashara za kuongoa mazingira. Biashara hizi zinategemea kuuza mbegu za nyasi zilizovunwa kwenye soko la ndani. Lengo ni kuboresha fursa za kiuchumi kwa jamii za wenyeji wakati wa kurejesha mandhari iliyoharibika.

Mbali na mapato ya ziada kwa wanawake na kijani kibichi  katika maeneo makavu, mradi huu pia husaidia kudumisha nyasi za asili za nyanda za asili ambazo mara nyingi hupuuzwa na maendeleo duni kwa soko na uhifadhi.

FAIDA YA HIFADHI YA BENKI YA MBEGU

Kwa wanawake
Kwa mazingira

KWA WANAWAKE

Kuuza nyasi na mbegu za nyasi zilizovunwa kutoka kwenye hifadhi ya mbegu za nyasi hutengeneza chanzo cha mapato kwa wanawake ambao wanasimamia benki za mbegu za nyasi.

Mapato haya hutumika kama njia mbadala ya kujipatia riziki, na kuwafanya wanawake wawe huru zaidi. Inaweza kusaidia wanawake kulipia ada ya shule, huduma za afya na kusaidia familia zao. Watu wengine ndani ya jamii wanaona mafanikio ya hifadhi ya mbegu za nyasi, ikiwapatia wanawake hadhi ya juu ndani ya jamii yao.

woman grass seed banks

KWA MAZINGIRA

Nyasi zilizopandwa katika hifadhi ya mbegu za nyasi huvutia wadudu na wanyama wadogo.

Kurudi kwao kunachochea kupona kwa mfumo wa ikolojia na inasaidia mimea katika maeneo ya karibu kuanza kukua pia. Mbegu za nyasi ambazo zinauzwa kwa miradi mingine ya urejeshwaji wa mazingira, zitaongeza kukijanisha maeneo mengine pia. Kwa mfano ndani ya miradi yetu ya makinga maji!

Grasses grass seed bank
grass seed bank
bee hive

Using bees to scare TEMBO

Tembo wanapenda kula nyasi za hifadhi ya mbegu za nyasi.

Kwa bahati mbaya, hii inasababisha uharibifu wa uzio uliotumika kulinda nyasi na nyasi zenyewe. Lakini Okoa Tembo ilikuja na suluhisho la ubunifu: kutumia mizinga ya nyuki katika uzio wa hifadhi ya mbegu za nyasi! Tembo wanaogopa nyuki. Wakati wanapojaribu kuingia kwenye hifadhi ya mbegu za nyasi, nyuki kwenye mizinga wataamka na kutisha tembo  waende mbali.

Faida nyingine kubwa kwa vikundi vya wanawake wa Kimasai ni uzalishaji wa asali. Wanawake wamefundishwa jinsi ya kutunza mizinga hii na jinsi wanaweza kuvuna asali. Kwa kuuza asali hutengeneza kipato cha ziada!