HATUA 1: Chagua
Chagua visiki hai ambavyo ungependa kuvitunza.
Anza kurudisha rutuba katika shamba lako kwa kufuata maelezo, video, mabango na redio, vyote hivi vipo hapo chini!
Njia ya Kisiki Hai imeitwa ‘Mkombozi wa mazingira’ hasa katika maeneo kame, kwa sababu kuu nne:
1. Gharama nafuu,
2. Endelevu,
3. Rahisi kwa mtu yeyote,
4. Matokeo ya muda mfupi.
Elewa faida za Kisiki Hai na jinsi ya kutumia mbinu hii ya kukijanisha.
Chagua visiki hai ambavyo ungependa kuvitunza.
Chagua maotea machache yenye ubora zaidi kutoka kwenye kisiki na yakate maotea yaliyobaki.
Weka alama kwenye maotea uliyochagua kwa kufunga kitambaa chenye rangi inayoonekana ukiwa mbali.
Tunza visiki vyako katika kipindi chote cha mwaka.
1. CHAgua: chagua visiki unavyotaka kutunza;
2. POgolea: chagua maotea machache yenye ubora Zaidi kutoka kwenye kisiki na yakate maotea yaliyobaki;
3. Alama: Weka alama kwenye maotea uliyochagua kwa kufunga kitambaa chenye rangi inayoonekana ukiwa mbali;
4. TUnza: Tunza visiki vyako katika kipindi chote cha mwaka!
Kumbukumbu rahisi: CHAPOA TU!
Wakulima wenzako wengi walianza kurudisha uoto wa asili, hivyo kuboresha ardhi yao. Hii inamaanisha wewe ni sehemu ya harakati kubwa ya kurudisha uoto wa asili! Hongera! Kwa Pamoja tunaweza kufanya Dodoma kuwa bustani ya Eden.
Jalome Sailowa mkulima kutoka Kijiji cha Mnyakongo mkoani Dodoma anasema:
“Tumekuwa tukikata miti kwa ajili ya kupata nafasi kwa ajili ya kilimo. Matokeo yake ni kumekuwa na upungufu wa uzalishaji na kuongezeka kwa mmomonyoko wa udongo. Kupitia LEAD Foundation na Justdiggit tumekubaliana njia za kurudisha uoto wa asili kama Kisiki Hai ambazo zinarutubisha udongo, zinaboresha ulinzi wa mazao na maisha kwa ujumla.”
Fanya makubaliano katika jamii. Uanzishwaji wa sheria ndogo ndogo na faini katika jamii kunaweza kusaidia kuzuia uchomaji wa misitu na kulisha mifugo hovyo.
Ndiyo, unaweza! Acha miti shambani kwako kwa mitindo miwili:
Ukichagua njia ya pili, zingatia yafuatayo:
Ushauri:
Matokeo na vipimo vya shamba yanaonyesha kuwa mavuno yanaongezeka baada ya kutumia njia ya Kisiki Hai!
Kwa kutumia njia ya Fanya Juu na Fanya Chini, una chimba makingamaji katika shamba lako ili kuvuna maji ya mvua.
Fanya Chini ni Kingamaji ambalo linachimbwa upande wa juu wa shamba, udongo uliochimbwa unawekwa upande wa chini ili kutengeneza tuta ambalo litazuia maji kutoka mlimani kuingia shambani ili kuzuia mmomonyoko wa udongo wenye rutuba.
Fanya Juu ni kingamaji ambalo linachimbwa upande wa chini wa shamba, udongo uliochimbwa unawekwa upande wa juu wa shamba ili kutengeneza tuta ambalo litasaidia kubakiza maji ya mvua shambani na kuongeza upatikanaji wa maji kwa mimea. Mwishoni inasaidia kukijanisha ardhi yako!
Kwa kushirikiana na Farm Radio International na Dodoma FM tumetengeneza vipindi vya redio kwa ajili ya mkulima, ambavyo vimerushwa katika mkoa mzima wa Dodoma. Katik hivi vipindi unajifunza kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, faida za Kisiki Hai na jinsi ya kukitumia. Kipindi hiki kina mahojiano, igizo, vichekesho na maswali kutoka kwa wasikilizaji. Tunakutakia usikilizaji mwema.
Sikiliza vipindi 16 hapo chini!