KUKIJANISHA AFRIKA NA KUPOOZA SAYARI YETU

Linapokuja swala kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, sote tuna kazi ya kufanya na tunakuwa tarehe ya mwisho kufanya.

Tunahitaji kuanza kubadili mabadiliko ya hali ya hewa kufikia mwishoni mwa muongo huu. Habari njema ni kwamba tayari tumeanza. Tayari tumefanya athari kubwa kwa miradi na kampeni zetu, lakini pamoja na wewe tunaweza kuzidisha hii, kukijanisha Afrika na kusaidia kupooza sayari nzima.

Angalia athari ambazo tumefanya hadi sasa na ujifunze juu ya athari chanya tunazofanya kwa kufanya ardhi kavu tena kuwa kijani. 

ATHARI
YETU

>430,000

Hekta chini ya urejesho wa ardhi

18.7 million

Miti million 18.7 imerejeshwa

450.000

Makinga maji ya nusu mwezi 450.000 yamechimbwa

291 million

Watu million 291 wamefikiwa ulimwenguni na kampeni zetu za uhamasishaji

20

Benki ishirini za mbegu za nyasi

TAYARI TUMERUDISHA HEKTA >430 ZA ARDHI

Pamoja na mamilioni ya wakulima na wafugaji, tunarejesha hekta elfu >430 za ardhi kavu, iliyoharibika. Kurudisha uoto  kuna athari chanya  kwa hali ya hewa, mazingira na bioanuwai, kwa watu na maisha yao.

Kenia_Kuku_Before-After (2)

TUMEREJESHA ZAIDI YA MITI MILLIONI 18.7 NDANI YA MIAKA nne

Tunarudisha maotea ya miti yaliyosahaulika kwa kutumia mbinu iitwayo Kisiki Hai. Hii ni bora zaidi kuliko kupanda miti mpya!

Kwa kuhuisha miti hiyo, tunaweza kurejesha maeneo yaliyoharibiwa na kuyafanya maeneo haya kuwa ya kijani na ya baridi tena.

2_techniques_landscape restoration_what we do_Justdiggit_Kisiki Hai_mnya_Tanzania

TUNA DAWA ZAIDI YA VISIMA ELFU 450

Makinga maji kama tunavopenda kuyaita “Dunia inatabasamu” ni mashimo ya nusu duara yanayotumika kuvuna maji ya mvua.

Yamechimbwa katika miradi yetu katika Afrika ili kuvuna maji ya mvua ambayo yangeweza kupotea kwa kupita katika ardhi kavu isiyo na kitu. Kwa kuchimba makinga maji. Tunaweza kukijanisha eneo kubwa ndani ya muda mchache, kunufaisha bio anuwai, asili, wat una na matokeo yake hali ya hewa.

.

6 juli 2020 bunds kenya drone (2)

HAMASISHA, UNGANISHA NA AMSHA

Ikiwa unataka kufanya mabadiliko ya ulimwengu, unahitaji kuwa kila mahali: habari, matangazo, vituo vya kijamii, mazungumzo, na zaidi ya yote katika mioyo na akili za watu. Ili kufanya hivyo, tunatumia nguvu ya vyombo vya habari na mawasiliano, kujenga utayari na uelewa na kuonyesha kuwa kwa pamoja tunaweza kuwa na athari chanya na muhimu kwa mabadiliko ya hali ya hewa.

Kampeni zetu za kimataifa za uelimishaji mtandaoni na nje ya mtandao zinatengenezwa ili kukuza njia za asili na kuhamasisha, kuunganisha na kuamsha kizazi kizima na kukuza harakati za kurudisha mazingira.

0(option 2)_header_farmers spread the word_dig in_Justdiggit_Kisiki Hai__roadshow_2018_marchaers_Dodoma_Tanzania

JUMLA YA BENKI 20 ZA MBEGU ZA MAJANI KATIKA MIRADI YETU

Ndani ya benki zetu za mbegu za nyasi, wanawake wa Kimasai hukua, huvuna, na kuuza nyasi (nyasi) na mbegu. Wanapata mapato kwa kuuza kwenye masoko ya ndani au kwa mashirika. Hifadhi za mbegu za nyasi huunda eneo lenye kijani  katika ardhi kame,  na nyasi ambayo wanawake huvuna ni chakula cha mifugo yao wakati wa kiangazi.

Kwa jumla tuna benki 20 za mbegu za nyasi huko Kenya na Tanzania.

5_Kuku_ Kenya_Work_What we do_Justdiggit_kenya_Kuku_grass_seed_bank_women_Kilimanjaro

FAIDA

Athari ya kuongoa ardhi

Katika miradi yetu, tunarejesha mandhari ya ardhi iliyoharibika kwa kutumia mbinu endelevu za usimamizi wa ardhi kama uvunaji wa maji ya mvua na Kisiki Hai. Kurejesha uoto kuna athari nyingi nzuri kwa hali ya hewa, mazingira na bioanuwai, kwa watu na maisha yao:

  • Joto
  • Uvunaji na uhifadhi wa hewa ukaa
  • Maji
  • Udongo
  • Kuongezeka upatikanaji wa mazao na kipato
  • Kuwawezesha wanawake
  • Ardhi bora ya malisho
  • Faida za bio anuwai

Joto

Uoto hupooza kwa njia kuu mbili: kwanza kwa kuunda kivuli na pili kupitia upumuaji (mimea inapotoa unyevu). Athari za mimea kwenye hali ya hewa ndogo zinaweza kuonekana wazi kwenye picha hii ya makinga maji.

Angalia tofauti ya joto kati ya mimea iliyo ndani ya makinga maji na sehemu nyingine zinazozunguka. Udongo ndani ya makinga maji umepoa zaidi sababu ya uoto ndani yake.

Water bunds landscape restoration Justdiggit Cooling effect vegetation

Uvunaji na uhifadhi wa hewa ukaa

Uoto pia una athari ya baridi kwa hali ya hewa ya kikanda na hata ya ulimwengu. Kwa kuhifadhi hewa ukaa kutoka hewani, kiwango cha hewa ukaa angani hupungua, na baadaye kupunguza athari ya gesi joto. Kwa kiwango kikubwa, hii ina athari chanya juu ya ongezeko la joto duniani.

3_Impact_what we do_Justdiggit_cooling_soil_temperature_vegetation

Maji

Mimea inatoa unyevu kwenda kwenye anga na  na hupooza hewa kwenye anga na kuongeza unyevu hewani. Kwa kiwango kikubwa kwenye, hii inasaidia kuunda mawingu na huongeza nafasi ya mvua, haswa mwanzoni na mwisho wa msimu wa mvua, kusaidia kurudisha mzunguko wa maji.

soil

Udongo

Kuongezeka kwa uoto  kunamaanisha  kuongezeka vitu vingi vya kikaboni, virutubisho zaidi na maji  kwenye mchanga. Mfumo wa mizizi ya mimea husaidia maji kuingia ardhini kwa urahisi zaidi na kwenda ndani zaidi, ambayo huongeza ukuaji wa miti na mimea.

Maji machache hupotea kutoka kwenye udongo kupitia njia za uvukizi kwa kivuli cha mimea, ambayo pia huongeza upatikanaji wa maji kwenye udongo. Mizizi ya mimea na miti pia husaidia kuhifadhi safu ya juu ya udongo wakati wa mvua kali, ambayo inazuia mmomonyoko wa mchanga wenye rutuba.

first vegetation

Kuongezeka upatikanaji wa mazao na kipato

Miradi yetu ya kukijanisha inasimamiwa na washirika wetu wa ndani za nchi zao na jamii zilizo katika maeneo hayo. Kwa kukijanisha mashamba yao wenyewe, wanaboresha ubora wa mchanga na upatikanaji wa maji, ambayo inaweza kuwa na athari chanya kwa mavuno ya mazao, kuongeza mapato yao na kuimarisha kujitolea kwao – na umiliki wa – mradi.

Fanya Juu Fanya Chini

Kuwawezesha wanawake

Ili kukuza usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa wanawake ni jambo muhimu katika kazi yetu. Nchini Kenya kwa mfano, tunaendesha ghala za mbegu za nyasi ambazo zinasimamiwa na kutunzwa kabisa na wanawake wa Kimasai. Katika eneo la mradi wetu nchini Tanzania, 50% ya Wakulima wetu wa mfano ni wanawake.

Landscape restoration - Justdiggit

Ardhi bora ya malisho

Kwa kuchimba makinga maji na kuboresha usimamizi wa malisho, maeneo yaliyoharibiwa yana muda wa kuboreka tena. Hii haifaidishi tu wanyama – mifugo na wanyama pori – lakini pia wafugaji wa Kimasai ambao hutegemea sana ng’ombe kama vyanzo vya chakula na mapato.

decorative image

Faida za bio anuwai

Bioanuwai ni muhimu kwa ajili ya ikolojia bora. Kwa kurudisha mimea na kuongoa mazingira, pia tunaboresha mazingira ya kuishi kwa aina nyingi za wanyama na mimea. Kwa upatikanaji zaidi wa maji na chakula, tunaona ongezeko la bioanuwai miongoni mwa mimea, wadudu, ndege na wanyamapori katika maeneo ambayo yamekijanishwa.

giraffe kuku

KUONGOA MANDHARI YA ARDHI

Kampeni zetu za uhamasishaji

Licha ya kufanya athari kwa miradi yetu ya kukijanisha, tunaendesha kampeni za kidunia kuelimisha mtandaoni na nje ya mtandao. Hizi zinakuza njia za asili na zinalenga kuhamasisha, kuunganisha na kuwezesha kizazi kizima, kukuza harakati za kurudisha mazingira.

MIRADI YETU