HAMASISHA UKIJANISHAJI

Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita tumefanikiwa kurejesha uoto kwenye maelfu ya hekta za ardhi, tumechimba mashimo ya kuhifadhia maji takribani nusu milioni, na tumerejesha miti milioni 18 kwa kutumia mbinu za ukijanishaji za teknolojia ya chini. Kimsingi, hii ni kazi nzuri sana, lakini bado haitoshi. Sasa ni wakati wa kuhamasisha zaidi kazi hii. Hebu tukujuze: mbinu za ukijanishaji za kidigitali.

Kuongezeka kwa simujanja zenye uwezo wa intaneti pamoja na huduma ya mtandao huo katika ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara, kunatoa fursa ya kutumia jimujanja hizo katika kuharakisha urejeshaji wa uoto. Hivyo, kwa kuandaa Ukurasa wa Kidigitali kwa ajili ya Ukijanishaji, tunaweza kuendeleza na kuongeza kasi ya ukijanishaji, hali inayotufikisha karibu na kutimiza lengo letu la kuwafikia wakulima wadogowadogo milioni 350.

decorative image

KIJANI

Kitovu cha jukwaa hili la kidigitali ni Kijani, hii ni app inayowapa wakulima walioko ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika, maarifa na ujuzi unaohitajika kwa ajili ya kukijanisha ardhi zao kwa ufanisi. Aidha, wanaweza kufuatilia masomo ya kidigitali yenye mbinu zilizothibitishwa ili kukijanisha ardhi zao na kuboresha maisha yao.

Kipekee kabisa, tunaishukuru teknolojia ya GPS, kwani tunaweza kutoa ushauri mahususi kabisa kwa kila mtumiaji wa app, jambo linalotufanya tuelimishe wakulima wengi zaidi bila hata sisi kwenda katika maeneo yao. Kwa kutumia jukwaa hili, tunaweza kutumia vizuri fursa ya uvumbuzi mkubwa wa kiteknolojia katika kuendeleza mipango ya ukijanishaji inayotumia teknolojia ndogo.

“Mara nyingi mashirika hutoa elimu na kisha hutoweka, lakini app hii ni chaguo sahihi sana. Ninaweza kupakua app hii na inaendelea kubakia kwenye simu yangu. Sasahivi nina nafasi nzuri ya kujifunza leo na kesho,”

alisema mkulima kutoka kijiji cha Owerendeke mkoani Arusha, Tanzania

Nguzo zetu nne

Kila tunachokifanya, yaani mikakati yetu na mbinu zetu, hushirikisha watu. Hii ina maana kuwa, huwa tunamlenga mkulima mmojammoja na jamii kwa ujumla ambayo huwa na uwezo wa kubadilisha ardhi. Hata Jukwaa Letu la Ukijanishaji Kidigitali halina utofauti!

Huwa tunatumia kichocheo cha mabadiliko ya mazingira ambacho hujumuisha mambo makuu manne: hamasisha, elimisha, wezesha na sherehekea. Tukiwa na lengo la kuwezesha wakulima 350,000,000 kukijanisha ardhi zao!

HAMASISHA

Kwa kiasi kikubwa, tunahamasisha matumizi ya njia za kidigitali ili kuwafikia wakulima pande zote za Afrika. Hii itawatia moyo na kuwahamasisha watu ama katika kupakua app (bure kabisa) na kuanza kukijanisha, au kuisambaza kwa marafiki au ndugu ambao ni wakulima.

Inspire

ELIMISHA

App yetu itatuwezesha kutoa mafunzo binafsi (ya mtu mmojammoja) kwa wakulima pamoja na ushauri kuhusu ukijanishaji. Kwa kutumia mbinu za ufundishaji kwa njia ya mtandao kama vile masomo ya hatua kwa hatua, wakulima wanaweza kupata maarifa na ujuzi wote unaohitajika ili kuweza kukijanisha ardhi zao kwa ufanisi.

Educate

WEZESHA

Tunawasaidia wakulima katika kutumia mbinu walizojifunza, na tunatumia mbinu ya uwezeshaji wa jamii ili kuhakikisha majirani zako mashambani wanahamasika na wao kujiunga. Pia, tunaandaa michezo mbalimbali ya kuigiza katika app yetu ili kuongeza matokeo mazuri.

Activate

SHEREHEKEA

Tunaweza kuufanya mfumo wa ufuatiliaji wa matokeo ya ukijanishaji yaliyofikiwa na wakulima ukawa unajiendesha wenyewe katika app hii. Pia, kuonesha na kusherehekea mafanikio na rafiki zako ni rahisi sana, hii ni kutokana na ushirikiano uliopo na majukwaa mengine ya mitandao ya kijamii.

Celebrate
Partner up Digital Regreening Platform

UKIJANISHAJI HUFANYIKA KWA PAMOJA

Tunaamini wazi kwamba, ushirikiano mkubwa unahitajika miongoni mwa miradi, mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali, serikali pamoja na mtu mmojammoja ili kukamilisha mabadiliko ya mahitaji ya sayari yetu. Ndiyo maana, tutaendelea kuwekeza katika upanuzi wa faida za miradi na app yetu kwa kukuza mtandao wa ushirikiano na wenyeji pamoja na mahusiano mazuri na wakulima wenyewe.

Kadiri tunavyoweza kusukuma maendeleo na kuharakisha juhudi zetu za kuongeza kasi mapema, ndivyo tutakavyoweza kufikia wakulima milioni 350 kwa haraka zaidi na kuwapa maarifa ya kukijanisha ardhi zao sambamba na kuongeza uwezo wao wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

"WAKATI MABILIONEA WA TEKNOLOJIA WAKIENDA SAYARI YA MIRIHI, SISI KIPAUMBELE CHETU NI ‘KUOKOA DUNIA’. KUPITIA TEKNOLOJIA, TUNAWAWEZESHA WAKULIMA MILIONI 350 KUKIJANISHA AFRIKA."

Carl Lens
Carl Lens Mkuu wa Kitengo cha Ukijanishaji Kidigitali

Wasiliana nasi!

Name

KUWA SEHEMU YA SULUHISHO LA KIDIGITALI

Mnamo tarehe 8 Agosti, 2024 tutakuwa tumeshazindua Kijani nchini Tanzania; hata hivyo, hatuna mpango wa kuishia hapo. Tunataka kuifanya iwe ni app itakayotumiwa na kila mkulima barani Afrika! Unaweza kushirikiana nasi kwa kutuwezesha kifedha, au kwa kutupa ujuzi wako, kuungana nasi au kuwa na shauku ya tunachokifanya. Usisite kuwasiliana nasi ili uwe sehemu ya harakati zetu za ukijanishaji kidigitali. 

Carl Lens

Carl Lens

Mkuu wa Kitengo cha Ukijanishaji Kidigitali