Nini maana ya uvunaji wa maji ya mvua?

Uvunaji wa maji ya mvua ni mbinu ambayo inazuia maji ya mvua kutiririka hovyo.

Badala yake, maji hukusanywa na kuhifadhiwa, kwa hivyo yanaweza kutumiwa na mimea, wanyama au watu.

Uvunaji wa maji ya mvua hufanywa zaidi katika hali ya hewa kame au yenye  nusu ya ukame, kwani maeneo haya yana kiwango cha chini cha maji kwenye udongo. Hii inasababisha upungufu wa maji kwa wanadamu, wanyama na mimea. Kuna njia mbili tofauti ambazo maji ya mvua yanaweza kuvunwa. Ya kwanza ni kutumia mikakati ya usimamizi wa udongo ambao unawezesha kuvuna moja kwa moja maji ya mvua ndani ya udongo. Hii inazuia maji kutiririka na huongeza upenyezaji kwenye mchanga. Inawezekana pia kuvuna mvua kwenye sehemu moja na kuihifadhi mahali pengine. Kwa mfano, kukamata maji ya mvua kutoka juu ya dari na kuyahifadhi ndani ya tenki. Maji haya hutumiwa zaidi kwa kumwagilia mazao au kunywa.

UMUHIMU NA ATHARI

Kwanini uvunaji wa magi ya mvua ni muhimu?
Ipi ni Athari ya uvunaji wa maji ya mvua?

KWANINI UVUNAJI WA MAJI YA MVUA NI MUHIMU?

Uvunaji wa uliopitiliza, mabadiliko ya hali ya hewa na ukataji wa miti husababisha upanuzi wa maeneo yenye jangwa na yenye nusu jangwa.

Hasa maeneo yaliyo hatarini , kama Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, inakabiliwa na athari mbaya za ukame na jangwa. Ukame huu husababisha uhaba wa maji kwa wanadamu, wanyama na mimea. Athari hii inaongezewa na ukweli kwamba mvua imekuwa kubwa zaidi. Kwa sababu maji mengi yanashuka mara moja, maji hayana wakati wa kupenya  kwenye udongo, na kusababisha mtiririko wa maji. Karibu na upatikanaji wa chini wa maji ndani ya udongo, hii husababisha mmomonyoko wa tabaka la juu la ardhi yenye rutuba ya udongo na  kuleta mafuriko. Kiasi cha maji kuwa chini  na kupungua kwenye udongo wenye rutuba hufanya iwe ngumu kukuza mazao, na kusababisha uhaba wa chakula kwa jamii za wenyeji. Hii inaweza kusababisha njaa. Kwa sababu kilimo mara nyingi ndio chanzo kikuu cha mapato, inaweza pia kusababisha umasikini.

Rainwater harvesting

IPI NI ATHARI YA
UVUNAJI WA MAJI YA MVUA?

Kwa kuvuna maji ya mvua, mmomonyoko na mafuriko yanaweza kuzuiwa.

Kwa kuongezea, uhaba wa maji ndani ya udongo unaweza kuongezewa, kupunguza ukame. Kuzuia kuondoa tabaka la juu lenye rutuba kwa na kuongeza unyevu wa udongo kuna athari kadhaa nzuri. Mazao yanaweza kupandwa tena, ikitoa chakula na pesa kwa jamii za wenyeji. Mimea mingine pia itaanza kushamiri tena, na kusababisha  kukijanisha  maeneo yenye jangwa au nusu jangwa . Kukijanisha  inakuza ufyonzwaji wa hewa ya kaboni, kupooza udongo na huchochea mzunguko wa maji wa ndani, na kuongeza upatikanaji wa maji kwenye udongo hata zaidi.

 

Landscape restoration - Justdiggit
Bund with rainwater

MAKINGA MAJI

Je! Justdiggit inatekeleza vipi uvunaji wa maji ya mvua?

Ili kuvuna maji ya mvua katika maeneo ya mradi nchini Tanzania na Kenya, Justdiggit hutumia mkakati wa usimamizi wa udongo ambapo makinga maji ya nusu mwezi huchimbwa. Makinga maji yanaweza kuvuna maji ya mvua, na kupunguza maji yanayotiririka. Hii inazuia mmomomyoko wa tabaka la juu lenye rutuba ya udongo. Kwa kuongezea, kwa kuvuna maji ya mvua, inawezesha zaidi kujipenyeza kwenye udongo, na kuongeza upatikanaji wa maji ndani ya ardhi. Hii inawezesha mbegu ambazo bado ziko kwenye udongo kukua, na kusababisha kijani!

Ni nani Justdiggit?

Na Jinsi gani Justdiggit wanasaidia kupambana na kutoa gesi ya kaboni na kupoooza sayari?

Justdiggit ni shirika la Uholanzi likiwa na lengo la kurejesha mifumo ya mazingira iliyoharibika kwa kukuza, kuanzisha na kufadhili mipango mikubwa ya urejesho wa mazingira ndani ya Afrika. Miradi yetu ya kukijanisha husaidia kurejesha ulinganifu wa maji kwenye udongo na kurudisha mimea, ambayo ina athari nzuri kwa hali ya hewa ya eneo , inaongeza usalama wa maji na chakula na inakuza bioanuwai ndani ya maeneo ya mradi. Ndani ya miradi yetu tunafanya kazi pamoja na washirika wa ndani na jamii. Jamii zilizohusika moja kwa moja zinanufaika na programu zetu tunapounda mazingira bora ya kuishi na kuongeza maendeleo ya uchumi. Njia yetu ya kipekee ni mkakati wa vyombo vya habari na mawasiliano, unaojumuisha mawasiliano na vyombo vyote vya habari vinavyopatikana kwa kiwango cha mitaa, mkoa, kitaifa na kimataifa. Pamoja na kampeni hizi za vyombo vya habari zilizodhaminiwa, tunakusudia kukuza athari ya programu za urejesho wa mazingira, na hivyo kuunda harakati za kurudisha mazingira, na kukuza kukijanisha barani Afrika.

poster