![decorative image](https://justdiggit.org/wp-content/uploads/2024/08/Kijani-newsitem.jpg )
Shirika la Justdiggit lazindua app ya Kijani ili kuongeza kasi ya ukijanishaji kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika
Kazi
Kurejesha nyanda za malisho zilizoharibiwa na kuhamasisha matumizi endelevu ya ardhi
Pamoja na Jumuiya ya Wamiliki wa Ardhi ya Kusini mwa bonde la ufa tunarejesha nyanda za malisho zilizoharibiwa katika Mkoa wa Kusini mwa bonde la Ufa na kuhimiza jamii kutekeleza tamaduni ya matumizi endelevu ya ardhi. Kwa kurudisha uoto na kulinda nyanda za malisho tunaweza kuboresha maisha ya jamii ya Wamasai na kusaidia wanyamapori wanaoishi katika eneo hilo.
Eneo la Kusini mwa bonde Ufa ni sehemu ya Bonde la Ufa Kusini, lililo karibu na mpaka wa Tanzania. Eneo hilo liko karibu na hifadhi kubwa mbili za wanyamapori – Serengeti-Mara na Kilimanjaro Mkuu-Amboseli-Tsavo – na inasaidia baadhi ya wanyama wenye utajiri zaidi duniani. Ni nyumbani kwa wafugaji wa Kimasai: jamii ya kuhamahama ambayo chanzo chake kikuu cha mapato na maisha ni ufugaji. Kwa sababu ya ukame unaoendelea, malisho ya mifugo kupita kiasi, na ongezeko la aina mbalimbali za hatari za mimea vamizi, maeneo ya malisho na vyanzo vya maji kwa mifugo yao vinapungua. Wakati huo huo, wanyamapori katika eneo hilo pia wanajitahidi kujikimu.
Wakati wa kuchukua hatua! Pamoja na mshirika wa SORALO tunatekeleza mbinu mbalimbali za kurejesha mandhari ili kurudisha uoto endelevu katika eneo hilo na kuondoa viumbe vamizi. Kwa kukuza mazoea ya matumizi endelevu ya ardhi miongoni mwa jamii, tunalenga kuboresha ubora wa nyanda zao za malisho. Hii itasababisha usalama zaidi wa chakula na maji, lishe zaidi kwa mifugo yao, na mapato zaidi kwa jamii zinazoishi katika eneo hilo. Kwa kuongezea, itasababisha makazi bora kwa wanyama wanaoishi katika mkoa huo. Kwa kiwango kikubwa, kufanya ardhi iliyoharibiwa kuwa ya kijani kibichi kuna athari ya kupoeza kwa hali ya hewa (ya ndani).
za ardhi zinazoendelea kuboreshwa
Matuta ya kuvunia maji yamechimbwa
Hifadhi za mbegu za nyasi
Lita za mji zilizohifadhiwa 2023
Fanya Juu na Fanya Chini
Kwa kushirikiana na wakulima na wafugaji, tunaboresha maelfu ya hekta za ardhi kame na iliyoharibiwa. Urejeshaji wa uoto umekuwa na matokeo mengi chanya katika tabianchi, mazingira na bayoanuwai, kwa watu na maisha yao kwa ujumla.
Matuta ya kuvunia maji (au kama tunavyopenda kuyaita: “tabasamu la dunia”) ni makingamaji yenye umbo la nusu duara ambayo hutumika kuvunia maji ya mvua.
Matuta haya yanachimbwa katika maeneo mbalimbali ya mradi barani Afrika ili kuvuna maji ya mvua ambayo vinginevyo yangetiririka na kupotea katika ardhi kame na tupu. Kwa kuchimba matuta ya kuvunia maji, tunaweza kukijanisha eneo kubwa zaidi kwa muda mfupi, na kunufaisha bayoanuwai, uoto, watu na – hatimaye tabianchi yetu.
Katika hifadhi zetu za mbegu za nyasi, wanawake wanapanda, wanavuna na wanauza nyasi (nyasi kavu) na mbegu. Wanajipatia kipato kwa kuziuza kwenye masoko yao au katika mashirika. Hifadhi za mbegu za nyasi hutengeneza kichaka cha kijani jangwani, na nyasi kavu wanayoyavuna akina mama hutumika kama chakula cha mifugo yao nyakati za ukame.
Uuzaji wa nyasi na mbegu za nyasi zilizovunwa kutoka kwenye hifadhi za mbegu za nyasi huwatengenezea kipato wanawake wanaotunza hifadhi hizo. Kipato hiki hutumika kama mbadala wa kuendesha maisha, na kuwafanya wanawake wasiwe tegemezi.
Jumla ya wanawake 80 wanajihusisha na hifadhi hizi za mbegu za nyasi.
Miongoni mwa faida za kurejesha uoto ni kwamba hutengeneza hali ya unyevunyevu zaidi katika anga. “Kutengeneza” uoto: huzalisha unyevunyevu angani na kupoza hali ya hewa. Kwa kiasi kikubwa, unyevunyevu husaidia kutengeneza mawingu na kuongeza uwezekano wa mvua, hususan mwanzoni na mwishoni mwa msimu wa mvua, na kusaidia kurejesha mzunguko wa maji.
Fanya Juu na Fanya Chini ni mbinu za kuvunia maji ya mvua. Wakulima huchimba mitaro kwa kufuata kontua katika mashamba yao ili kuzuia mmomonyoko na kuvuna maji muhimu ya mvua katika ardhi yao.
Kwa ujumla, zaidi ya kilomita 8 za mitaro zimechimbwa na wakulima Mkoa wa kusini mwa bonde la ufa.
Kwa kutekeleza mbinu mbalimbali za kurejesha mandhari tunarudisha uoto endelevu kwenye nyanda za malisho. Mbinu zilizopendekezwa ni:
Mbinu zilizotekelezwa zitasaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo wenye rutuba na kurejesha ulinganifu wa maji katika udongo.
Pia tutavuna maji kama suluhisho la usimamizi wa malisho. Kwa kutoa maji mengi zaidi nje ya maeneo ya malisho yaliyohifadhiwa, mifugo inaweza kuwekwa nje ya maeneo hatarishi kwa muda mrefu, na hivyo kuacha muda zaidi kwa mimea kurejea.
Hifadhi ya mbegu za nyasi ni sehemu ndogo ya ardhi ya jumuiya ambayo hutumiwa kwa ajili ya uzalishaji wa nyasi na mbegu za nyasi.
Hifadhi ya mbegu za nyasi zinasimamiwa na kudumishwa na vikundi vya wanawake wa Kimasai. Mara baada ya nyasi kuota kikamilifu, nyasi huzalisha mbegu za nyasi ambazo huuzwa na wanawake katika masoko ya ndani au kwa miradi mingine ya kukijanisha. Hii inamaanisha mapato zaidi kwa wanawake na kijani zaidi katika maeneo mengine, hali ya ushindi!
Ili kuhakikisha uendelevu wa miradi, tutatengeneza mpango wa usimamizi wa malisho pamoja na mshirika wetu wa ndani na jamii.
Lengo ni kuzuia malisho ya mifugo kupita kiasi katika maeneo muhimu na hatarishi ya malisho.
Mradi huo ulioko kusini mwa bonde la ufa ni sehemu ya kilmo cha kijani cha badae cha kijani, juhudi kutoka RAIN, MetaMeta na Justdiggit.Kilimo cha kijani ya baadaye ni mradi wa miaka minne unaolenga kuonyesha jinsi gani katika mandhari tatu tofauti kabisa, katika nchi tatu tofauti (Uganda, Ethiopia na Kenya), kilimo cha urejeshaji wa uoto kinaweza kuwanufaisha wakulima na mazingira. Kwa kuchanganya uwekezaji katika kuongoa wa uoto wa asili na usimamizi wa mandhari, kujumuisha kilimo cha kurejesha uoto, na kuimarisha minyororo ya thamani ya ndani, mradi unalenga kufanya uchumi wa vijijini kuwa na nguvu zaidi.
Kinachofanya programu kuwa maalum ni ukweli kwamba kila shirika sio tu linaendesha programu yao ya ndani, lakini pia inasaidia programu zingine ndani ya utaalam wao wenyewe. Lengo kuu la programu ni kujenga mustakabali wa mandhari ya kijani kwa wengi, haswa kwa wanawake na vijana, katika sehemu tofauti za Afrika Mashariki. Mpango huu unaungwa mkono na IKEA Foundation.
Tazama filamu ya utangulizi Kilimo cha Kijani ya Baadaye hapa.
Ili kuona kuona kutatua jinsi suluhisho zinazotegemea asili zinavyobadilisha, kanuni za ikolojia, na maisha ya jamii kwa ujumla, ni muhimu macho yako mwenyewe.
Lakini hapo ndipo changamoto inapoanza: hatuwezi kuleta watu wote duniani kwenye miradi yetu. maana tumeunda suluhisho hili la kupita kupitia uzoefu wa mwingiliano. Tumefanya maajabu ya miradi yetu ya kijani kibichi yaweze kufika moja kwa moja kwako—popote ulipo!