Kisiki Hai Kuongoa Mandhari ya Ardhi

2022
2023

KWA JINSI GANI TUNAIRUDISHIA
ARDHI MITI?

Kutoka kwenye Kisiki kuwa Mti.

Shida kubwa ya ukataji miti, uharibifu wa ardhi, na ongezeko la joto ulimwenguni imesababisha kuongezeka kwa ardhi kavu na isiyo na rutuba katika nchi nyingi za Kiafrika. Kuna mamilioni ya visiki hai katika mashamba, maeneo ya malisho na misitu iliyoharibika barani Afrika na ikiwa na uwezo wa kukua tena kuwa miti, ikiwa itapata nafasi.

Tunarudisha mashina ya  miti iliyosahaulika kwa kutumia mbinu iitwayo Kisiki Hai. 

Kwa kuhuisha miti hiyo, tunaweza kurejesha maeneo yaliyoharibiwa na kuyafanya maeneo haya kuwa ya kijani na ya baridi tena.

Man performing Kisiki Hai

Nini Maana ya Kisiki Hai?

Kisiki Hai ni mbinu ya kukuza miti tena na kuwezesha  mimea mipya inayotokea kwa njia ya asili kukua. Kulikuwa na miti mingi katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Mingi kati ya hio ilikatwa zamani kutumika kama kuni, mbao, kwa ajili ya uzalishaji wa mkaa au kutoa nafasi kwa kilimo kwani wakulima walikuwa wakiamini kuwa ardhi nzuri ni ardhi wazi.

Kwa mbinu ya Kisiki Hai mashina ya miti hii hupata nafasi ya kukua kuwa miti halisi tena. Inajumuisha mchakato wa kuchagua, kupogolea na kutunza.

CHAPOA TU

Hatua nne za Kutunza Kisiki Hai

1. CHAgua: Chagua mashina unayotaka kuyatunza;

2. POgolea: Chagua maotea bora miongoni mwa yaliyopo kwenye shin ana kata mengine yote;

3. Alama: Weka alama kwa kufunga kitambaa cha rangi inayoonekana vizuri katika maotea unayotaka yakue;

4. TUnza: Endelea kutunza miti kwa kipindi chote cha mwaka!

Urahisi wa Kukumbuka tunaita  CHAPOA TU!

poster

Angalia video ya maelekezo

FAIDA ZA KISIKI HAI

Kuhuisha miti ina Faida kadhaa:

* Miti inayochipua tena na mimea inayotokea kwa asili ina nafasi nzuri ya kuishi kwani ni aina ya asili na tayari imezoea hali ya hewa ya eneo hilo;

* Mfumo wa mizizi ya miti iliyokatwa tayari iko na hufikia kina kirefu cha udongo. Hii inawawezesha kufikia maji ya chini ya ardhi, na kuongeza kuongeza uwezo wakustahimili;

* Wakati wa kuhuisha miti au kulinda mimea inayotokea  kwa asili, aina mbalimbali za viumbe mara nyingi hukua tena. Hii inasababisha kuongezeka kwa bioanuwai.

Kisiki Hai Treecovery

FAIDA YA MITI

Kivuli cha miti husaidia kupoza hali ya hewa . Hii hupunguza   athari ya joto kwa mazao na kuzuia uvukizi wa maji kutoka ardhini.

* Miti husaidia kuhifadhi maji kwenye udongo. Pamoja na kupungua kwa uvukizi wa maji kutoka ardhini, hii inasababisha kuongezeka kwa upatikanaji wa maji kwa mimea mingine.

* Majani yanayoanguka kutoka kwenye miti hufanya kama mbolea, na kuongeza rutuba ya udongo.

* Miti hupunguza kaboni, na kupunguza kiwango cha gesi ya kaboni kwenye anga na hivyo kupunguza athari ya hewa ukaa.

* Miti huvutia kila aina ya ndege na wadudu. Ndege hawa hula matunda ya miti, hueneza mbegu kupitia kinyesi chao, na hivyo kueneza kukijanisha.

MBINU NYINGINE ZA KUKIJANISHA