TUPO KATIKA MDORORO WA DUNIA KUHUSU
HALI YA MAZINGIRA

Sayari yetu inapata joto wakati idadi ya binadamu ikiongezeka.

Katika maeneo yenye hali ya ukame Afrika, mabadiliko ya hali ya hewa, uharibifu wa ardhi, na uvunaji wa rasilimali za mazingira kupita kiasi unasababisha joto kupanda, ardhi kukauka na mchanga wenye rutuba kumomonyoka. Hii inasababisha shida kubwa kama vile ukame uliokithiri na njaa. Kwa bahati nzuri, kuna suluhisho! Ikiwa tutarudisha asili kwa kiwango kikubwa cha kutosha tunaweza kufanya athari chanya katika mabadiliko ya hali ya hewa. Sasa ni wakati wa kuchimba na kuongeza kiwango. Mbio zinaendelea.

Degraded Ecosystem - Drought - Africa _ Justdiggit

UPOTEVU WA ARDHI YENYE RUTUBA

Kila mwaka, ulimwengu hupoteza hekta milioni 12 za ardhi yenye uzalishaji.

Ikiwa na matokeo makubwa na yanayofika mbali! Ikiwa ni pamoja na kushuka uzalishaji wa mazao, kuongezeka kwa mvutano juu ya maliasili, uhamaji wa kulazimishwa na kudhoofisha uthabiti kwa mabadiliko ya hali ya hewa.

Tunachohitaji kufanya ni kuweka kijani kibichi kwenye ardhi kavu, iliyoharibika. Wakati mimea inapotea, mzunguko wa uharibifu wa mazingira haraka unachukua nafasi: mawingu hayaji na anga huwaka. Wakati mvua inanyesha, udongo hauwezi kufyonza maji, na kusababisha mafuriko na uharibifu zaidi wa udongo. n.k

"DUNIA YETU INAKAUKA, KWA BAHATI NZURI SULUHISHO NI RAHISI.”

Desmond Tutu, Mlezi wa Justdiggit
Kisiki Hai before
Kisiki Hai after

Sehemu hio hio wakati wa kabla na baada ya kutumia njia za asili kuongoa ardhi, Tanzania

KUONGOA
ARDHI NDIO
SULUHISHO

Kwa bahati nzuri, tunaweza kubadilisha mambo!

Utafiti unawema kuwa kwa kutumia matumizi ya njia ya asili zenye gharama nafuu, tuna uwezo wa kuzuia ongezeko la joto duniani kwa asilimia 37%! Ushirikiano wa Ulimwenguni wa Kurejeshwa kwa Mazingira ya Msitu ulikadiria kuwa, ulimwenguni, zaidi ya hekta billioni 2 za misitu na ardhi iliyoharibiwa inaweza kurejeshwa, eneo kubwa la mara mbili ya Ulaya!

Iweke kwa urahisi, hakuna wakati wa kupoteza. Tunataka kuvunja mduara huu mbaya wa ukame na mmomonyoko  kwa kuanza kurejesha  hekta billioni 2 za ardhi kupitia mjia ya kukijanisha. Uoto  hufyonza hwa ukaa, huwezesha maji kushikwa kwenye udongo, huleta kivuli na hupunguza uvukizi: kwa kifupi, hupooza sayari. Ndio jinsi tunavyorejesha ardhi kavu na iliyoharibika: kwa kuifanya kuwa kijani tena. Kwa kurudisha mimea tunarudisha ikolojia pia, kuboresha hali ya maisha, na kutengeza upatikanaji wa maji zaidi na usalama wa chakula.

MUONGO
WA KUONGOA
IKOLOJIA

Kwa kupitia umoja wa mataifa

Kulingana na sayansi, muongo huu ni muhimu katika vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa. Ndio sababu Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa umetangaza 2021-2030 Miaka kumi juu ya Urejeshwaji wa Mfumo wa Ikolojia: harakati ya kimataifa ya kuongeza juhudi za kurejesha mazingira yetu.

Faida za miaka kumi zitaonekana kupitia lenzi ya 17 ya Umoja wa Mataifa

Malengo ya Maendeleo Endelevu” . Mifano ni njia za asili za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, usalama wa upatikanaji wa maji na chakula na uhifadhi wa bioanuwai.

Justdiggit ni mshirika rasmi katika muongo mmoja juu ya Urejeshwaji wa Ikolojia na kazi yetu ina athari chanya angalau katika malengo 8 kati ya 17 ya mpango wa maendeleo endelevu.