NINI MAANA YA KUKATA MITI?

Ukataji miti ni mchakato wa kukata misitu na baada ya hapo ardhi hutumiwa kwa sababu zisizo za misitu.

Misitu inajumuisha asilimia 31 (hekta bilioni 4.06) za ardhi ya dunia. Hali ya kuwa, kwa sababu ya ukataji miti, idadi hii inapungua haraka. Inakadiriwa kuwa kila mwaka hekta milioni 10 za misitu hupotea, ambapo hekta milioni 3.9 barani Afrika.

Sio tu kwenye misitu miti hukatwa kwa kiwango cha kuongezeka sana , pia kwenye uoto wa nyasi na maeneo ya mashambani upotezaji wa miti ni mkubwa.

Dry - Soil - Kenya - Justdiggit

NINI KINASABABISHA UKATAJI WA MITI?

Ukataji miti na upotezaji wa miti husababishwa sana na shughuli za kibinadamu. Miti hukatwa ili kutoa nafasi kwa kilimo au malisho ya mifugo, viwanda na  uchimbaji madini au hupotea kwa sababu ya shughuli  nyingine za  misitu. Upotezaji wa miti pia unaweza kusababishwa na michakato ya asili kama vile moto wa mwituni. Kwa sababu ya ongezeko la joto ulimwenguni njia hii ya asili ya ukataji miti iliongezeka haraka kwa miaka iliyopita.

MATOKEO YA UKATAJI WA MITI

Gesi ya kaboni
Kupotea kwa bioanuwai
Athari kwa watu
Mmomonyoko wa udongo

Gesi ya kaboni

Miti hufyonza hewa ya kaboni kutoka hewani na kuitunza kaboni ndani yake.

Kukata miti na kuchoma miti kunasimamisha ufyonzwaji wa hewa ya kaboni  na kuirudisha angani, na kuharakisha ongezeko la joto duniani.

Drought - Africa - Justdiggit - Tree

KUPOTEA KWA BIOANUWAI

Ukataji wa miti na upotezaji wa miti kwenye uanda wa nyasi  na mashambani pia husababisha kupungua kwa bioanuwai.

Misitu ni nyumba ya viumbe vingi, ambapo haviwezi kuishi bila uwepo wa miti. Pia kwenye maeneo ya uanda wa nyasi na mashambani, miti ni muhimu kwa viumbe hai vingi.

giraffes

ATHARI KWA WATU

Sio mimea na wanyama tu wanategemea uwepo wa miti.

Wakulima kwa mfano, pia hutegemea faida za miti: Kivuli cha miti huzuia uvukizi wa maji kutoka ardhini, na kuongeza upatikanaji wa maji kwa mazao kwenye shamba. Kivuli pia hulinda mazao kutokana na kuchomwa na jua.

Shadow - Tree - Africa - Justdiggit

MMOMONYOKO WA UDONGO

Mfumo wa mizizi ya miti huzuia mmomonyoko wa udongo wenye rutuba.

Mmomonyoko wa udongo ni moja wapo ya athari mbaya sana za kukata miti na husababisha uharibifu mkubwa wa ardhi unaosababisha maeneo kuwa wazi na makavu.

Erosion gully Tanzania
Women practicing Kisiki Hai

JINSI TUNAVOWEZA KUKABILIANA NA UKATAJI WA MITI?

Kuna njia kadhaa za kuondoa ukataji miti na upotezaji wa miti kwenye uanda wa nyasi na shambani. Njia moja ni kulinda misitu na miti ambayo bado ipo. Kwa kuunda maeneo ya uhifadhi, miti inalindwa kutokana na mazoea ya kukata miti na shughuli zingine za kibinadamu zinazosababisha upotezaji wa miti.

Lakini, kulinda miti haitoshi. Ili kurudisha usawa duniani, inahitajika kurudisha miti ambayo hapo zamani ilikuwepo. Kwa kupanda miti mpya, inayoitwa pia upandaji miti, misitu inaweza kurejeshwa. Njia nyingine ni kuibadilisha miti ambayo hapo zamani ilikuwepo. Hivi ndivyo tunafanya katika mradi wetu huko Dodoma, Tanzania. Kwa msaada wa mbinu inayoitwa Kisiki Hai, wakulima wanarudisha  miti kwenye ardhi zao ambayo huongeza idadi ya miti.

NI NANI HAO Justdiggit?

Na Jinsi gani Justdiggit wanasaidia kupambana na kutoa gesi ya kaboni na kupoooza sayari?

Justdiggit ni shirika la Uholanzi likiwa na lengo la kurejesha mifumo ya mazingira iliyoharibika kwa kukuza, kuanzisha na kufadhili mipango mikubwa ya urejesho wa mazingira ndani ya Afrika. Miradi yetu ya kukijanisha husaidia kurejesha ulinganifu wa maji kwenye udongo na kurudisha mimea, ambayo ina athari nzuri kwa hali ya hewa ya eneo , inaongeza usalama wa maji na chakula na inakuza bioanuwai ndani ya maeneo ya mradi. Ndani ya miradi yetu tunafanya kazi pamoja na washirika wa ndani na jamii. Jamii zilizohusika moja kwa moja zinanufaika na programu zetu tunapounda mazingira bora ya kuishi na kuongeza maendeleo ya uchumi. Njia yetu ya kipekee ni mkakati wa vyombo vya habari na mawasiliano, unaojumuisha mawasiliano na vyombo vyote vya habari vinavyopatikana kwa kiwango cha mitaa, mkoa, kitaifa na kimataifa. Pamoja na kampeni hizi za vyombo vya habari zilizodhaminiwa, tunakusudia kukuza athari ya programu za urejesho wa mazingira, na hivyo kuunda harakati za kurudisha mazingira, na kukuza kukijanisha barani Afrika.

poster