Kisiki Hai Kuongoa Mandhari ya Ardhi

2022
2023

KWA JINSI GANI TUNAIRUDISHIA
ARDHI MITI?

Kutoka kwenye Kisiki kuwa Mti.

Shida kubwa ya ukataji miti, uharibifu wa ardhi, na ongezeko la joto ulimwenguni imesababisha kuongezeka kwa ardhi kavu na isiyo na rutuba katika nchi nyingi za Kiafrika. Kuna mamilioni ya visiki hai katika mashamba, maeneo ya malisho na misitu iliyoharibika barani Afrika na ikiwa na uwezo wa kukua tena kuwa miti, ikiwa itapata nafasi.

Tunarudisha mashina ya  miti iliyosahaulika kwa kutumia mbinu iitwayo Kisiki Hai. 

Kwa kuhuisha miti hiyo, tunaweza kurejesha maeneo yaliyoharibiwa na kuyafanya maeneo haya kuwa ya kijani na ya baridi tena.

Man performing Kisiki Hai

Nini Maana ya Kisiki Hai?

Kisiki Hai ni mbinu ya kukuza miti tena na kuwezesha  mimea mipya inayotokea kwa njia ya asili kukua. Kulikuwa na miti mingi katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Mingi kati ya hio ilikatwa zamani kutumika kama kuni, mbao, kwa ajili ya uzalishaji wa mkaa au kutoa nafasi kwa kilimo kwani wakulima walikuwa wakiamini kuwa ardhi nzuri ni ardhi wazi.

Kwa mbinu ya Kisiki Hai mashina ya miti hii hupata nafasi ya kukua kuwa miti halisi tena. Inajumuisha mchakato wa kuchagua, kupogolea na kutunza.

CHAPOA TU

Hatua nne za Kutunza Kisiki Hai

1. CHAgua: Chagua mashina unayotaka kuyatunza;

2. POgolea: Chagua maotea bora miongoni mwa yaliyopo kwenye shin ana kata mengine yote;

3. Alama: Weka alama kwa kufunga kitambaa cha rangi inayoonekana vizuri katika maotea unayotaka yakue;

4. TUnza: Endelea kutunza miti kwa kipindi chote cha mwaka!

Urahisi wa Kukumbuka tunaita  CHAPOA TU!

poster

Angalia video ya maelekezo

poster

FAIDA ZA KISIKI HAI

FAIDA YA MITI

MBINU NYINGINE ZA KUKIJANISHA